Kwanini Ukubali kudanganywa!

Kwanini Ukubali kudanganywa!

Saint_Mwakyoma

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Posts
865
Reaction score
1,208
Kwenye maisha tunayoishi kuna changamoto nyingi tunazipitia . Changamoto hizo nyingine hutupandisha kutoka sehemu moja na kutuweka kunako nafasi fulani na nyingine huturudisha nyuma kabisa kwenye nyanja mbalimbali kiuchumi,kibiashara, kimahusiano na hata kiimani

Kiini kikubwa haswa cha changamoto hii ya kurudishwa nyuma huwa ni kudanganywa kibaya zaidi sio tu sisi binafsi muda mwengine , jamii nzima , ukoo ,umoja fulani na hata taifa pia huwa tunapitia kudanganywa (kutapeliwa,kulaghaiwa,kusalitiwa nk)

Sasa swali linakuja kwanini ukubali kudanganywa?

Kila mtu anaweza akawa na mbinu zake binafsi za kumsaidia kugundua yupo kwenye mtego wa kudanganywa au la.
Embu tusaidiane mbinu hizi za kukataa uongo uongo wa kutukwamisha kwenye nyanja mbalimbali au shuhuda (experience) jinsi kudanganywa kulipo kukwamisha au kukurudisha nyuma kimaendeleo fulani .

" fool me once shame on you, fool me twice shame on me,its your fault to be fooled again"
 
kwa pis kali huchomoi unaweza ukajiona upo peke yako kumbe kuna timu nzima ya mpira mna pasiana kwa zamu!
Mzee ukitoa kwa pisi kali ambako umerudisha mpila kwa kipa ....ushawai kutana na kudanganywa ambako umejalibu kusahau ila bado ukikumbuka ni kama visu vinakuchoma hivi ?
 
Kudanganywa hakukwepeki labda fanya ukishajua unadanganywa zijue mbinu za kwenda nao vizur uongo na wewe muongo ukitaka kudanganya jitahd matukio yaendane
 
Back
Top Bottom