BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Mie nilikuwa nasikia kijiweni kila siku. Umeona alichoandika kule Jambo Forums yule Mzee ES? Nikiuliza washkaji wananitolea nje hawaniambii kitu wanasema we tinga jambo forums ukamsome Mzee ES. Ilikuwa inaniudhi sana mpaka nikahisi walikuwa wanaitangaza Jambo Forums. Basi siku moja nikatinga humu kuja kumsoma Mzee ES AKA Le Mutuz hahahahahaha lol! Basi nikawa natafuta kusoma posts za Le Mutuz tu lol! wakati ule alikuwa anashusha nondo zenye shibe basi nikajikuta nimelowea. Wakati ule wanachama hata 200 hawafiki akina dada hata 10 hawakufika. Basi kulikuwa na mkakati humu wa kuongeza idadi ya akina dada. Leo hii wamejaa tele toka wanachama mia na kitu sasa tunakimbizana na 400k si hapa hata kidogo.