Hivi vitabu ukivisoma ukiwa open mind utaona mengi yakushangaza!!
Ni hatua ngumu sana kama umekulia katika vitabu hivi toka utotoni kuvitazama kwa fikra huru.
Sasa hapo kuna ugumu gani kwenye hiyo aya.
Kwa wasio mwamini Mungu kama yupo, na hiyo aya haipo vilevile, haina maana yoyote.
Kwa wanaoamini Mungu wanaelewa tena kwa wepesi kabisa kuwa Mungu ndiye chanzo cha kila kitu.
Huyo Shetanini aliumbwa na Mungu.
Mungu anauwezo wa kumfanyia ubaya mtu yoyote pamoja na Shetani mwenyewe.
Kabla ya kukufanyia ubaya Mungu huwa anakueleza mapema kuwa ukifanya hivi utaadhibiwa hivi.
Adam alishatahadharishwa kuwa
"walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika"
Mwanzo 2 : 17.
Mungu alimkataza huku akiwa amempa matunda mengi ya kula.
Baadae Adamu akala lile tunda sasa kilichofuata ni adhabu ya kifo.
Hapa nani wa kulaumiwa ?
Mungu alimruhusu Shetani kumpa magonjwa Ayubu huku alisha mfundisha Ayubu kuto mkufuru Mungu.
Hivyo ni Mungu ndiye aliyeruhusu Ayubu kujalibiwa.
Ni kweli Shetani siyo chanzo cha ubaya kwani hata Shetani mwenyewe anasubiri kufanyiwa ubaya na Mungu kwa kuunguzwa kabisa siku za hukumu ya kiyama.
Mungu aliiharibu kwa gharika dunia ya Nuhu na pia akaichoma Sodoma na Gomola huu ni ubaya ambao hata Shetani hauwezi kuufanya kwani hajaruhusiwa na Mungu kuufanya.
Mungu alifanya hivyo baada ya watu wa huko kufanya uovu wa kupindukia na hivyo kuadhibiwa na Mungu.
Lakini tunasoma Nuhu na Lutu ambao walikuwa wanaishi kwa kufuata maagizo ya Mungu waliokolewa na Mungu mwenyewe.
Shetani alipewa uhuru wa kuwashawishi wanadamu kuacha kuzitii amri za Mungu kwakuwa Mungu ndiye Muasisi wa Utawala wa Democrasia akamruhusu wakati amesha waeleza watu kuwa wasimtii Shetani.
Pia Mungu alisha wapa uwezo wanadamu wa kumkataa Shetani, na amewatahadharisha watu ambao kwa hiari yao wata zikataa amri Mungi kuwa mwisho wa siku atawateketeza kwa Moto pamoja na Shetani Mwenyewe.
Sisi binadamu kwakuwa ni dhaifu hatuna jinsi zaidi ya kuamua hatima yetu kwa matendo yetu wenyewe.
Tungekuwa na nguvu tungetenda dhambi na mwisho wa siku tungekataa kwenda motoni.
Lakini kwakuwa sisi hatuna nguvu ya kuweza kuyakataa maamuzi ya Mungu,
Na kwakuwa tunapenda kuishi milele kama Mungu alivyotuahidi basi TUNALAZIMIKA kutenda mema ya Mungu ili tuendelee kuishi maisha ya milele.
Kwahiyo hakuna ukakasi hapo
Wema wote na Ubaya wote ni Mungu ndiye anayeruhusu utokee.
Ni sawa na mtu akikuambia ukinywa hii sumu hakika utakufa.
Kama utakunywa na ukafa utamlaumu aliyekuonya isinywe ?
Kama niyeye aliyeitengeneza hiyo sumu hapo mbaya ni nani sasa?
Kama ndio au siyo mimi sijui.
Mwanadamu umepewa maarifa ili uweze kuchagua, mema na mabaya ni kipi anachotaka kimtokee.
Je
1. Unataka kutenda mema ili uishi maisha ya milele mbingumi baada ya kifo ?
2.Unataka kutenda mambo aliyokatazwa na Mungu ili Mungu akuue kabisa kwa kukuchoma moto baada ya kifo chako cha mwili ?
Ni juu yako kuchagua.
Nawasalimu wote mnaotia mashaka juu ya uwepo wa Mungu.
Ndugu zangu Mungu yupo na anataka tizitii amri zake na hatuna namna kwani
"Hatuna Pa Kukimbilia Asitukamate"
Kwa sasa ni hiari yetu kuamua kwamba tunatambua uwepo wake au la.
Kwamba tunazifuata amri zake au la.
Ndiyo maoni yangu
Che mittoga.