Kwanini unaingia katika ndoa?

Dogoli kinyamkela

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
618
Reaction score
1,440
KWANINI UNAINGIA KATIKA NDOA?

NDOA: Ni makubaliano ya muingiliano utakaohusisha hisia,

Muingiliano utakao husisha miili ya watu wawili walioamua kuanzisha Familia ya Baba na Mama..
Kwa maridhiano ya wazazi wao...!

Je ndoa kwani lazima iidhinishwe na mchungaji au sheikh au Askofu?
Hapana sio Lazima.

Kukishakua na maridhiano ya watu waliokubaliana kuishi Kama mume na mke kwa kupenda kwao
Wanaweza kua ni wanandoa kabisa..!

Haya mengine ni nyongeza tu za kimaslahi Kidini na kisheria..haimanishi bila hayo. Hawa watu hawawezi kua wana ndoa.

SASA

Kijana unataka kuoa kwasababu zipi?

Je ni kwasababu umri umeenda na wenzako wote,wana vyeti vya ndoa toka makanisani mwao,na kwa mkuu wa wilaya?

Je unaoa kwasababu ndugu wamekusema sana?

Unaoa kwasababu ni utaratibu umeukuta basi nawewe huna budi kufuata mkumbo.?

Au unaoa kwasababu mama yako anataka mjukuu wa kupakata?

Au unaoa kwasababu ni muda umefika nawewe uishi?

Unaoa kwasababu unataka nawewe uchangiwe,na kupokea zawadi Kama unavyowatoleaga wengine?๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿ˜Ž๐Ÿ˜Ž

unaoa kwasababu kuna mikataba na vitu vingine lazima ujaze marital status??๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿ˜Ž๐Ÿ˜Ž

Basi kama unaingia kwenye ndoa kwasababu Kama hizo na zifafanazo na hizo basi tambua...
Ndoa sio kwajili yako maana itakushinda๐Ÿฅต๐Ÿฅธ๐Ÿฅธ

INGIA

Kwenye ndoa kwasababu umependa wewe mwenyewe toka rohoni mwako.๐Ÿ˜Ž

Kiasi kwamba uko tayari kuijaza dunia kwa maongezeko ya uzao..Na utawala utakaoambatana nao,
Yaani kusiwe na sababu yoyote zaidi ya upendo kati yenu.. Pesa isiwe sababu, Mali zisiwe sababu...basi mtafurahia.๐Ÿฅธ๐Ÿฅธ

BINTI

Unaingia kwenye ndoa na huyo mwanaume kwasababu zipi?

:je ni kwasababu marafiki na mashosti zako wote wameolewa,wako kwenye majumba yao...nje wanakuchekea je unajua wanayoyapitia ndani?๐Ÿฅบ๐Ÿ˜Ž๐Ÿ˜Ž

: je unaolewa kwasababu unataka uwatambishie wanawake wenzako,kua umefanya party kwenye ndege,kwenye boat?
Umefunga harusi iliyo gharimu mamilion ya fedha?๐Ÿ˜Ž๐Ÿ˜Ž

: Au unaolewa kwasababu kwenu ni hohe hahe,yaani pako pako tu sasa umeamua kuolewa ili huyo bwana umtegemee akafanye mabadiliko kwenu...?
Kwanini mama yako hakukupatia huyo baba tajiri? Kama hio ndio target yako kwenye ndoa?๐Ÿฅธ
: unaolewa kwasababu umeshahangaika na wanaume vya kutosha sasa unatafuta mtu wa kukufichia aibu.?๐Ÿ˜Ž
: Au unaolewa ili nawewe upate heshima kua ni mkewa fulani?

KAMA unaolewa kwasababu hizo na nyingine zifananazo na hizo tambua fika hiyo ndoa,
Hutaiweza utatumika tu ndivyo sivyo.

OLEWA

Kwasababu umempenda mtu toka moyoni.

Kwasababu umekubali kua msaidizi wa kweli kifikra,kiuchumi,na kijamii kwa huyo mwanaume.๐Ÿฅธ

olewa kwasababu umekubali kwa moyo wako wote kua unaenda kumsaidia huyo jamaa kuijaza dunia...maana yake hautakua na sababu ya kumsumbua na kumnyima huyo bwana ngono yake๐Ÿ˜Ž๐Ÿ˜Ž
Kwakua ni wajibu wenu kupeana.๐Ÿ˜Ž

ELEWA HILI

Huyo unayemuona ni Handsome..kuna siku linaweza kutokea la kutokea uso na umbo likaharibika....lakini hilo halitakuteteresha maana umependa utu wake.๐Ÿ˜Ž

Unaweza kumwoa binti kwa shape yake lakini baada ya kujifungua,umbo lake likabadilika na kuharibika lote...lakini hill likawa halikusumbui tena maana ukipenda utu wake umbo halitazitatanisha hisia zako kwake๐Ÿฅธ๐Ÿ˜Ž

KUNA
Watu waliolewa kwababu walitaka wawakomoe Ex zao,lakini walikimbia baada ya kuona giza tu huko.

Wako walioolewa kwasababu zao binafsi...

Lakini walipoenda kukosa watoto walikimbia.

Walipofika na kukutana na maneno ya wifi zao waligeuka.

Wengine walipofika huko walienda kugombanisha watu na mama zao.
Wengine walipofika huko walienda kudhoofisha uchumi wa mwanaume ili kuimarisha uchumi wa nyumbani kwao...

Pasipo kujua kua kwake ni kwa huyo mwanaume. Na kile anachofanya kwao ni kuingilia majukumu ya baba yake tu.

Ahsante.

Content created by : Dogoli kinyamkela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ