Kwanini Unaishi !

Kwanini Unaishi !

Tunaishi ili tujifunze.
Naam kujifunza utake usitake utajifunza tu ndio maana hata kuku anajua kuparua ili kupata chakula sababu alimuona mzazi wake anafanya hivyo (monkey see, monkey do) kwahio inabidi ajifunze ili aweze kupata basic needs....
Au kama mtoa mada unavyosisitiza basi: mimi ninaishi ili nijifunze.
Naam hilo ni jema sana na nadhani ukiwa na mapenzi ya kujifunza basi utakuwa mtu mwenye furaha sababu kila siku utakuwa na purpose yaani kitu cha kufanya hence utakuwa haupo bored na challenge hazitaisha sababu ukiwa open minded utakubali kusikiliza hoja za huku na kule.... (mfano kipindi cha age of enlightenment, watu walikuwa ni watu wa kudadisi na ku-debate hoja tofauti)
Maana nikiangalia maisha ni mtiririko wa kutolewa katika uzoefu mmoja kupelekwa kwenye uzoefu mwingine.

Mwisho wa siku nafsi yangu iupate uzoefu kamili wa kuishi kwa amani na mapendo na nafsi za watu wengine.

Nahisi hili ni kusudi la msingi la maisha ya utu wetu wa ndani. Experience!

Au nyie ndugu zangu mnadhani ni kwa nini mtoto asizaliwe na kufa tu? Ni nini cha muhimu anachosubiri hadi miaka 8090704020 etc. Au kipi hasa ni cha tofauti anachokuwa nacho mtu wakati anazaliwa? Na wakati anakufa!?
Kwa logic hii wenye changamoto ya akili / kujifunza basi wasingeishi ? Binafsi nadhani to each his/her own hata mtu asiye na akili ya kupembua mambo bado yeye matamanio yake ni muda wa chakula ufike labda apate mlo au kwenye akili yake anachokiona hakipo sawa akiweke sawa (na ni nani wa kusema yeye hana akili na sisi ndio tuna akili ? Ignorance a Bliss huenda yeye moyo wake una furaha kuliko mtu anayejua mambo).....
Seee!! Experience........ what has he/she learned nakaribisha michango
Experience comes with age na inaweza ikawa mbaya, nzuri au potofu...., lakini naweza ninakubaliana na wewe kwamba tunaishi leo ili tuwe bora kuliko tulivyokuwa jana (ingawa ubora kwako huenda usiwe ubora kwangu)
 
Kwa upande wangu ninaishi ili kizazi kijacho kuishi.
Kuishi haimaanishi ujue lengo la kuishi maana kuishi kwenyewe ni kusudio tosha bila kujali unaishije.

Kuna watu wanaishi kwa makusudio ya watu wengine yaani nje kabisa na vile wao wanataka kuishi. Aidha wazazi, mke, marafiki, ajira, siasa, mapenzi, mazingira. N.k
Hivyo unajikuta maisha yanakuwa yamejaa maswali mengi, stress, vurugu za kila aina sababu tu haupo katika kusudio lenyewe la kuishi.

Ukiwa mtoto maisha ni raha sana lakini kadri unavyokua na kujaribu kujua mambo mengi ndio njia ya kuipoteza furaha.

Hii ni kwa sababu matamanio yachukua nafasi yake na kitu Tamaa hakijawahi kumuacha mtu salama hakijitoshelezi ni endelevu. Hapa huwezi kuwa na furaha mpaka mauti yanakukuta.
Ni kweli ulioyasema " tunaishi ili kizazi kijacho kiweze kuishi.

Mfano rahisi nitaongelea kitu kinaitwa "Maamuzi'' tunayoyafanya haijalishi hatayakiwa madogo au makubwa yanadetermine maisha ya kizazi kijacho.

Kijana wa mwaka 1950 anaamua kununua ardhi (maamuzi) kwa shughuli za kilimo na makazi, anakuja kurithi mjukuu mwaka huu 2024 na kuendeleza shughuli za kilimo na makazi kama alivofanya babu yake.

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli ulioyasema " tunaishi ili kizazi kijacho kiweze kuishi.

Mfano rahisi nitaongelea kitu kinaitwa "Maamuzi'' tunayoyafanya haijalishi hatayakiwa madogo au makubwa yanadetermine maisha ya kizazi kijacho.

Kijana wa mwaka 1950 anaamua kununua ardhi (maamuzi) kwa shughuli za kilimo na makazi, anakuja kurithi mjukuu mwaka huu 2024 na kuendeleza shughuli za kilimo na makazi kama alivofanya babu yake.

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
Ukweli ni kwamba hili suala lina majibu tofauti na kila mtu ana motivation tofauti..., Lakini mara nyingine kuna wajibu wa mtu au msukumo wa jamii unayomsukuma mtu kufanya jambo fulani sio sababu anapenda bali jamii ndio inamtaka afanye hivyo...

Huenda ni kweli Babu yako alianzisha shamba ila Je alianzisha shamba kwanini ?
  • Sababu anapenda Kilimo au ni katika kutafuta security yake (kutafutia juani ili alie kivulini)
  • Sababu anapenda ku-accumulate wealth yaani ndio hobbie yake kwahio ana live the dream
  • Sababu apate ujiko mtaani kwamba fulani na yeye ni mtu?
  • Ili wajukuu zake wapate makazi ?
Nachotaka kusema ni kwamba wengine wanapata mahitaji yao kwa kufanya kile wanachopenda LAKINI wengi wanachofanya hawakipendi bali ni njia tu ya kujipatia mahitaji, hivyo ni kama wapo Gerezani....
 
Swali sio kwamba Kwanini watu wanaishi nauliza kwanini wewe Unaishi ?

Dhumuni la swali ni kujaribu kueleweshana huenda watu tumesahau kwamba Binadamu tupo tofauti chema kwako ni kibaya kwa mwingine...; Ila mwisho wa siku kila mtu anahitaji Kusudi (Purpose); kitu kinachomsukuma kuamka asubuhi na kufanya anachofanya..., Iwe ni kumridhisha mwenza, kuhudumia familia, kutoa elimu, kutoa Tiba, Kutetea wenye shida, Kula Bata n.k.

Kama kila mtu ana kusudi (purpose) inayomfanya kufurahia maisha, kama Jamii hatuoni kwamba tunapotoka tunapodhani watu tunaishi ili kupata Pesa ?; Yaani mtu hapendi kujichanganya na watu tunamwambia awe daktari sababu inalipa au mwanasiasa Je huyu atafurahia maisha wakati anachofanya sio kusudi lake ?

Iweje Msanii / Muimbaji aseme kazi ya Usanii hailipi wakati hata asingelipwa angeweza kuifanya Bure ?!!!

Binafsi nadhani maisha ni simple sana watu ndio wanaya-complicate kwa kutaka kuishi kwa jicho la Jamii linavyokuona na sio wewe binafsi unataka nini au kutokujua ni nini tunataka, na kudhani the Grass is Greener on the Other Side - Hivyo kusahau kuishi bali kutumia muda wetu hapa duniani tuki-chase an ILLUSION....
Amka utafute hela mzee, achana na ndoto za kimaskini.

Kutokubadili nguo ni purpose? Kuishi kwa shida (bila Huduma muhimu) ni purpose?

Pesa sio kila kitu, lakini ukiwa na pesa unakua na options.

Mf. Unataka kusafiri from Mwanza to dar.
== ukiwa huna pesa, moja kwa moja tunaweza kutabiri utatumia usafiri wa bus.

Lakini ukiwa na kibunda unakua na options, unaeza panda ndege, unaeza washa chombo yako e.t.c
 
Amka utafute hela mzee, achana na ndoto za kimaskini.
Hata unajua maana ya umasikini ? Kwahio kwako wewe umasikini ni lack of money ? Kudhani kwako pesa ni ndio alfa na omega ndio kupotoka kwako..., umasikini ni lack of resources zinazokufanya uwe depraved na basic needs; ukishapata basic needs kinachofuatia hapo sio the same kwa ila mtu
1733767371176.png



Kutokubadili nguo ni purpose? Kuishi kwa shida (bila Huduma muhimu) ni purpose?
Kwanini mtu habadilishi nguo ? Au kwanini mtu anavaa nguo in the first place ? Nguo purpose yake ni kujikinga na extremities na kama ndivyo na nguo hio ni safi basi inakidhi kigezo hicho..., ila kama ni sababu ya appearance basi mwingine anaweza kuona kuwa na nguo nyingi ni vulgarity na kuwa kwake nazo nyingi kila akizivaa anakuwa hana peace of mind...; Au mwingine anaweza kuona kuvaa kitambaa chenye chata ya Nike Addidas ndio amefika, wakati mwingine anaona kutoa Laki moja kwa nguo yenye value ya sumni sababu ya chata ni kuwa shortchanged..... Au kwa logic yako basi kungekuwa hakuna nudists au naturalists.

Na unapoongelea basic needs kuna feeling safe and secure, unaweza ukawa na pesa za kumwaga na unaishi kwenye nyumba ya dhahabu ambayo kwa macho ya wengi watakuona umefika, (lakini you don't feel safe and are full of stress) and by that token hauna peace of mind....
Pesa sio kila kitu, lakini ukiwa na pesa unakua na options.
Nope inawezekana unachotaka wala hakihitaji pesa wala kuwa kwako na pesa usiweze kupata unachohitaji..., inawezekana kuwa kwako na pesa kukakunyima hizo options..., and by the way like I said kuanzia mwanzo basic needs ni muhimu kwa kila binadamu sababu bila hizo then nothing else matters.., Na lazima ujue kwamba Ni vigumu kupata all that you want hata kama una pesa..., unaweza ukawa unataka kwenda mwezini lakini hata hicho chombo hakipo..., thus the happier person ni yule ambaye anaridhika na alichonacho au anacho anachokitaka... unaweza ukawa na Pesa nyingi ila unakaa Monaco na sababu pesa zako ni average kulinganisha na watu wa kule kwahio hata clubbing huwezi kwenda kwa kukosa nafasi na kila ukitaka kuingia ni fully booked wakati mwingine hata kwenda clubbing hataki na kusoma kwake novel ndio mpango mzima na anaisha kijijini kwenye natural air without pollution
Mf. Unataka kusafiri from Mwanza to dar.
Mwingine hata kusafiri hataki na alipo ameridhika thus anapata anachotaka na anaweza kutoka point A mpaka B kwa kufanya zoezi la kutembea....
== ukiwa huna pesa, moja kwa moja tunaweza kutabiri utatumia usafiri wa bus.
Mwingine basi ndio anapenda sababu kwake ni utalii na mwingine ingawa anapenda basi ila hana option sababu ni star au anajulikana sana hivyo akisafiri na wanajamii inakuwa kero au anasumbuliwa na hawezi kupata privacy, hivyo kupelekea kutokuwa hata na hio option..., Mwingine yupo kijijini ambapo kutoka point A mpaka B kwa siku ni rahisi na mwingine yupo New York, traffic congestion na pollution ndio order of the day na katika maisha yake anatumia robo tatu akiwa stuck in traffic (sio kwamba anapenda bali ndio hali halisi na yupo stuck in a rat race)
Lakini ukiwa na kibunda unakua na options, unaeza panda ndege, unaeza washa chombo yako e.t.c
Like I elaborated above wants zinategemea na mtu na mtu na unaweza ukawa na pesa na usiwe na options ya kupata unachotaka and vice versa...,

Pia kujikita kwenye usafiri (Au one category na sio Underlying Wants ambazo zina differ) you are missing the point.., Purpose ni kile ambacho unatamani na kukifukuzia kwahio the difference between happiness and being miserable ni acquirement ya hicho kitu, vingine vyote ni facilitators bahati mbaya watu wanadhani pesa ni main ingredient ya facilitation thus wanashangaa hata siku wakipata hizo pesa bado wapo miserable
 
Back
Top Bottom