Kwanini Unaogopa Kufa?

Kiukweli watu wengi wanaogopa kufa sababu wanadhani wataenda JEHANAM!!

Ingawa utasema unaogopa kufa sababu hujui uendako au labda familia utaiachaje, ila wengi wakiwaza ule moto wanaogopa(ambako wengi wanaona wanaqualify kuwa huko)

Wanaojiua wanakuwa wameamua kabisa hata moto uweje liwalo na liwe.

Jiulize mtoto mdogo asiyejua peponi na jehanam(ukiachilia mbali kufa) anaogopa kufa?
 
mimi kwa kweli naogopa,just because wanangu watalelewa na nani?lakini nikifikisha miaka 100 hivi,wala siogopi

we ndio muoga kweli kweli, miaka 100? yaani uko tayari kuishi kwa shida sababu ya uzee kuliko kufa mapema?
 
Mi nadhani wengi sio wanaogopa, bali hawataki kuziacha raha za dunia hii.
 
ni theory ngumu lakini urahisi wake unaweza ukaulinganisha na mfano wa mtoto aliyeko tumboni mwa mama anavyoogopa kuzaliwa ili aje katika hii dunia. Kwanza kwa uelewa wake japo anakuwa na hisia lakini hawezi kujua dunia hii ikoje kama sisi tusivyoweza kujua dunia inayokuja baada ya mauti ikoje!
 
Kitu cha muhimu cha kuogopa ni hofu yenyewe zaidi ya kifo,so inatakiwa ujue jinsi gani ya kupambana na hofu sio kifo
 
Kwahiyo kikubwa ni watu au maisha yako unayoacha ndio yanakutia hofu ila sio suala la motoni au peponi?

Kwa wale waumini wa dini wanaamini wanaweza kuepukana na motoni kwa maombi. Upo sahihi kuwa kinachoogopesha mara nying ni kujua kuwa utakufa kabla hujakamilisha malengo yako hapa duniani.
 
wazo la 'kukata roho' ndo linaniogopesha. Sijui kwanini (wala si hofu ya life after death), lakini kwa experience yangu nilivyoona watu wanavyokata kata roho, dah, sitaki kujiona in that situation.
I hope nife nikiwa usingizini/unconcious
 
WOGA huzalishwa na hofu juu ya kupata maumivu au mateso ya kimwili au kiakili/kiroho.
1. upo woga juu ya maumivu ya kukata roho au aina ya kifo! (linauhusiano kisayansi zaidi)
2. upo woga wa adhabu ya hukumu baada ya kifo! (hili la kiimani zaidi kuliko sayansi)
 
Kifo, kifo, KIFO!
Siogopi kifo kwa sababu za kiimani, nina uhakika nikifa sitajitambua, itakuw endless emptiness and unconscious! hakun moto wala mbingu, kimyaaaaa!
Mimi naogopa kifo kwa sababu bado ni kijana, dunia ina raha zake na malengo yangu hayajatimia, na hata malengo yakitimia bado ntaendelea kuogopa kifo kwa sababu kitanitenganisha na raha za matunda ya kazi zangu, familia yangu pia, watoto wangu ina maana sitawaona tena! Mke wangu, Masononeko yatayokuwa nyuma baada ya mim kufa.
 

Mtoto haogopi kuzaliwa mkuu, fahamu zake zinakuwa ndogo sana kiasi hawezi kuwaza kama unavyowaza wewe! Anapolia wakati wa kuzaliwa ni mchanganyiko wa maumizu ya kubanwa wakati wa kuzaliwa na mabadiliko ya ghafla ya mazingira na kupanua mapafu kwa mara ya kwanza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…