Kwanini unataka mtoto/ watoto?

Kwanini unataka mtoto/ watoto?

GAZETI

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
5,286
Reaction score
6,736
Ni kweli wapo ambao wamepata watoto kwa bahati mbaya, wengine walijaribu
hata kutoa mimba ikashindikana. Ninaowakusudia hapa ni wale ambao wamedhamiria
kupata hao watoto. Tena wengine wamethubutu hata kwenda kwa waganga.
Wako ambao wanasema wanataka watoto ili wawasaidie hapo baadae.

Nataka kujua kutoka kwenu kwanini unahitaji mtoto/watoto mpaka kufikia kukosa
furaha ndani ya mahusiano na mwenza wako?
Unataka akusaidie?
Ni pambo la nyumba?
Kwanini mtoto?
 
Tusipohitaji mtoto wewe saa hizi ungekua wapi ? Obvious usingekuwepo, nani angeandika hii thread yako? Na nani angeisoma? Watoto wa jana si ndiyo wakubwa wa leo ? M'buyu si ulianza kama mchicha ? Au ?
 
haya weweeeeee.........hebu jiulize kwa nini usiwe na mtoto wakati una ndoa halali_zaeni mkaongezeke na muijaze dunia
 
Bila watoto kutakuwa na Taifa hapo baadae???
Usidhani tutakuwepo milele. Sisi tutaondoka watoto ndio watakaoendeleza juhudi zetu.
 
Umeongea jambo la maana sana, so why uzazi wa mpango? maana
sisi katika familia yetu tuko kumi kwa mama, kwa baba tuko 27 Je kuna
tunaowanyima haki ya kuishi kama uliyoipata wewe?
 
Kwa hiyo kifupi tunafuata maandiko kwa mujibu wa Comment yako lakini
kuna ambao hawana maandiko na wamethubutu kuandika thread eti hakuna
Mungu. Kama wapo naomba wanijibu nao watoto ni wa kazi gani?
 
Bila watoto kutakuwa na Taifa hapo baadae???
Usidhani tutakuwepo milele. Sisi tutaondoka watoto ndio watakaoendeleza juhudi zetu.
Inaweza kuwa hiyo ndo sababu yako lakini kuna mahusiano yameingia
matatizoni au mpaka kuvunjika kisa mtoto hapo ndipo nilipo.
 
Tatizo ni pale tunapojibu kwa niaba ya wengine.
 
Inaweza kuwa hiyo ndo sababu yako lakini kuna mahusiano yameingia
matatizoni au mpaka kuvunjika kisa mtoto hapo ndipo nilipo.

Kwa ninavyojua Dhumuni kubwa la ndoa ni watoto. Lakini ikitokea bahati mbaya wasipopatikana isiwe sababu ya kuvunjika kwa ndoa.
 
Umeongea jambo la maana sana, so why uzazi wa mpango? maana
sisi katika familia yetu tuko kumi kwa mama, kwa baba tuko 27 Je kuna
tunaowanyima haki ya kuishi kama uliyoipata wewe?

Kwa sisi dunia ya 3 idadi kama yenu ndiyo inayotufaa au kupita hiyo! Tunahitaji sana "Rasilimaliwatu" ofcoz yasemekana ni 25% ya land yetu ndiyo tunaitumia kwa kilimo, the rest 75% hazitumiki coz hamna watu. Angalia China walipo kwa sasa kimaendeleo na vipi population yao!
 
Tusipohitaji mtoto wewe saa hizi ungekua wapi ? Obvious usingekuwepo, nani angeandika hii thread yako? Na nani angeisoma? Watoto wa jana si ndiyo wakubwa wa leo ? M'buyu si ulianza kama mchicha ? Au ?

Kwani wewe unadhani uwepo wako ni upendeleo na unafaidika nao?Mi ningefaidika sana kama nisingekuwepo humu kwenye unafki,umbea,roho mbaya,kijicho,vita na n.k!
 
Kwanza hakuna mtoto anaepatikana bahati mbaya,ngoja nione sababu zao!
Naungana na ww hakuna mtoto wa bahati mbaya hata siku moja,
Mpaka sasa sijafanikiwa kukutana na mtu aniambie mtoto wake ni wa bahati mbaya kwani nina majibu yao ya kutosha nasubiri siku mtu aniambie maneno hayo.
 
Kwa ninavyojua Dhumuni kubwa la ndoa ni watoto. Lakini ikitokea bahati mbaya wasipopatikana isiwe sababu ya kuvunjika kwa ndoa.

Sio kweli ndoa umeielewa vibaya, dhumuni sio kupata watoto, watoto ni baraka kutoka kwa Mungu. Dhumuni la ndoa ni kujipatia msaidizi na kuwepo watoto au wasiwepo ni sawa tu. Adam aliumbiwa msaidizi ila Mungu aliwaagiza wazae waongezeke wakaijaze nchi. Kuzaa ni sehemu ya uumbaji ya Mungu mwenyewe kupitia mwanadamu.
 
Binafsi naona watoto wana umuhimu sana kwangu,
Na namwomba mungu siku moja anipatie japo wawili,
Maisha yangu naamini hayatakamilika bila kuwa na watoto km wazazi wangu walivyonileta duniani,
Haka km itashindikana kuwa na wangu wa damu yangu basi nitaadapti na kutimiza lengo langu la kuwa na mtoto.
 
Kwanza hakuna mtoto anaepatikana bahati mbaya,ngoja nione sababu zao!
Ngoja nirekebishe lugha. Sijui niseme watoto wasiopangiliwa au wasiotarajiwa?
 
Kwani wewe unadhani uwepo wako ni upendeleo na unafaidika nao?Mi ningefaidika sana kama nisingekuwepo humu kwenye unafki,umbea,roho mbaya,kijicho,vita na n.k!
Duh, mkuu una msongo wa mawazo nini?
 
Naungana na ww hakuna mtoto wa bahati mbaya hata siku moja,
Mpaka sasa sijafanikiwa kukutana na mtu aniambie mtoto wake ni wa bahati mbaya kwani nina majibu yao ya kutosha nasubiri siku mtu aniambie maneno hayo.
Mimi nimewahi kukutana nae tena anasema kabisa amejaribu sana
kuitoa ile mimba ikashindikana.
 
Back
Top Bottom