LeBron TZ
Senior Member
- Sep 26, 2018
- 176
- 207
Habari za Mei Mosi wana JF wenzangu. Mimi ni mshabiki kindaki ndaki wa timu ya Yanga. Nilianza kuipenda Yanga kwa sababu mama yangu pia alikua mshabiki mzuri sana wa timu hii. Pia kulikua na mjomba wangu ambaye kipindi hicho mimi ni mtoto nilimuona kuwa alikua the brightest na tajiri sana ukilinganisha na wajomba zangu wote, sasa hivi ni marehemu Mungu amrehemu alipo. Alikua ni mshabiki mzuri na mwanachama wa Yanga.
Hicho kilikua ni kipindi cha utoto sijui A wala B. Nilipokua mkubwa sasa na uwezo wa kujenga hoja nikawa nao, nikaanza kuzichunguza timu hizi mbili either niendelee kushabikia Yanga au la kutonaka na facts; niache kufuata mama na mjomba niwe judge mwenyewe bila kufuata mkumbo, nikaona walikua sahihi kuwa wapenzi wa timu yetu hii ya wananchi.
Nilipitia historia ya timu zote mbili na nikaridhishwa sana na historia ya Yanga. Kwanza timu ya Yanga ndio ilianza kwanza na Simba ikafuata, ambapo Simba ilitoka ubavuni mwa Yanga. Kwa hiyo Simba ni kama mtoto wa Yanga.
Yanga ina vikombe vingi vya ligi kuu ya Tanzania, na pia H2H Yanga na Simba, Yanga imeifunga Simba mara nyingi zaidi toka timu hizi kuanzishwa.
Hizo ni baadhi tu ya sababu chache zilizonifanya niendelee kuwa mshabiki wa Yanga. Ingawa kwenye mashindano ya kimataifa wapinzani wetu Simba wamekua wakifanya vizuri zaidi yetu kwa muda mrefu, naona pia wananchi tumeamka baada ya kuweka historia mpya kabisa hiyo jana. Naamini huu ni mwanzo na mwendelezo mzuri wa Yanga ya kimataifa.
Kigezo pekee ambacho wapinzani wetu wamekua wakitutambia kwa muda mrefu sana, ingawa kwa upande wangu sioni sababu ya kutamba kufika nusu au robo fainali na kombe hujachukua.
Kwa ujumla timu hizi mbili kwa pamoja zimesaidia sana kukuza mpira wa Tanzania na kusababisha kutambulika kimataifa, mfano wa derby namba tano kwa bara la Africa.
Karibu shabiki wa Yanga na Simba useme kwa nini unaipenda timu yako na ulianza vipi kuwa mshabiki wa timu yako hiyo pendwa.