Kwanini unga wa ngano haupikiwi ugali?

Kwanini unga wa ngano haupikiwi ugali?

The Evil Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
6,017
Reaction score
19,506
Habari!

Naomba kujua kwanini unga wa ngano hua haupikwi ugali kama unga mwingine wa muhogo, mahindi nk.
 
Hivi ushawahi kupika Hata Maandazi au Chapati... Ukaona Huo unga Ukiuwekea Maji tu Unakuwaje
 
Huku kwetu "unga wa ngano" tunapikia ugali na uji... Au unga wa ngano upi unaozungumzia wewe ambao huwezi pika ugali
 
Unaweza kupikia ugali tu japo unachelewa sana kuiva na utausonga sana pia, maana ni mmwepesi mno, na ugali wake itabid usubir upoe kidogo ili ukuwe mgumu atleast.
 
Hiyo kwako tu,mbona sisi kwetu tunapikia ugali.
Kama huamini thibitisha mwenyewe kwa vitendo.
 
Mmenikumbusha pindi nasoma nilienda kupima unga
Bahati mbaya yule mwana mama akanipimia ngano
Wakati huo niliacha maji yanachemka
Nilipofika tu nikachota nikaweka mmh yani nilistuka kuona rangi
Nikahisi huenda huu unga wa mahindi kuna udaga ulikuwemo
Nilisonga lakini naona haueleweki ikabidi nimuite rafiki yangu
Kuja akaanza kushika unga akasema aise hii ni ngano
Ilibidi tuumwage ila ulikuwa ugali tu nilihofia kula huenda ukafunga haja
 
Mbona unga wa ngano unapika ugali vzur tuu mkuu
 
Back
Top Bottom