Kwanini unga wa ngano haupikiwi ugali?

Kwanini unga wa ngano haupikiwi ugali?

Ninachokwambia ni kweli kabisa, usiukoroge uji tho!
Uji koroga wa dona kama kawaida ila wakati wa kusonga ugali, changanya ngano(isokobolewa) na dona, inakuwa kama umeweka unga wa muhogo.

Ni mtamuuuuu.
Kwa hyo naweza kusaga ngano isiyokobolewa pembeni kisha nikachanganya unga wake na unga wa dona au lazima nichanganye vyote kwa pamoja ndio nisage?
 
Kwa hyo naweza kusaga ngano isiyokobolewa pembeni kisha nikachanganya unga wake na unga wa dona au lazima nichanganye vyote kwa pamoja ndio nisage?
Hata ukichanganya wakati wa kupika pia sio mbaya, vyovyote vile inafaa.
 
Changanya na dona, utakula ugali mwanana kabisa....ila peke yake sijawahi kujaribu....
 
MIHOGO UGALI.jpg
 
nenda makete taula ugali wa ngano
Makete tunatumia unga wa ngano kupika ugali, au unachanganya na viazi ulaya kupata ugali au unachanganya na viazi vitamu unapata ugali Fulani.

Kwa mtu wa kanda za Makete na Njombe, ugali wa ngano ni kitu cha kawaida, hasa Wakinga na wawanji.
 
Ugali_lishe huandaliwa kwa kuchanganywa kwa unga wa mahindi mtama ulezi michogo ngano au mchele ugali unakuwa mtamu sana unaweza kula bila mboga
 
Back
Top Bottom