A
Anonymous
Guest
Habari,
Naomba kufahamu ni kwa nini ushuru wa kusafirisha mazao unatofautiana kati ya halmashauri, huku tofauti hiyo ikiwa kubwa licha ya kuwa ni zao la aina moja.
Kwa mfano, kusafirisha mchele kutoka Mbeya au Iringa kwenda Dar es Salaam hutozwa kati ya Sh1,000 na Sh2,000 kwa kila kilo 100. Hata hivyo, kusafirisha mchele kutoka Morogoro kwenda Dar es Salaam hutozwa Sh4,000 kwa kila kilo 100.
Je, ni sahihi zao la aina moja kutozwa ushuru tofauti kulingana na halmashauri linakotoka? Ikiwa ndivyo, msingi wa utofauti huo ni upi?
Aidha, je, Serikali haiwezi kuweka viwango vya ushuru vinavyofanana nchi nzima kwa mazao ya aina moja, kama ilivyo kwa baadhi ya tozo, ada na leseni za biashara, ili kuondoa tofauti zinazowaongezea wafanyabiashara gharama na kuleta usawa?