Kwanini utalii wa ndani haupewi kipaumbele Tanzania

Kwanini utalii wa ndani haupewi kipaumbele Tanzania

Waziri1

New Member
Joined
Jan 24, 2025
Posts
2
Reaction score
1
Katika pitapita zangu za kufuatilia vivutio vingi vya Tanzania, na huduma zake nimegundua mambo kadhaa ya kushangaza sana.

Kwanza kabisa , Watanzania wengi hawapendelei kutembelea vivutio vyao vya utalii, wengi wao hawapo interested kabisa na utalii, hatuna culture ya kutalii na kiukweli wengi wetu hatuwezi kuafford utalii lakini pia hata wale ambao wanapenda kutalii na wanaweza kumudu gharama wengi sana huwa wanalenga kutalii nchi za nje (Watu wengi sana wamefika Dubai kabla ya Serengeti)

Lakini hata pale ambapo nilidhani kwamba hili ni tatizo la kitamaduni tu. hata nilipotembelea baadhi ya vivutio, nikaja kugundua kwamba hata kwa vivutio hivi vya utalii(Au huduma zinazozunguka vivutio hivi) mara nyingi hulenga wageni wa nje za nchi hadi muda mwengine kupelekea kufanya malipo kwa pesa za kigeni inaonesha kabisa kwamba Watanzania sio "Target Market" wa sehemu hizo

Sasa kijana mwenzenu nimebaki na maswali. Nini ni tatizo kwenye hii issue ya internal tourism. na ni jinsi gani tunatatua.
 
Kiukweli mm binafsi sina tu hela..
Mm pia hata ningekua na hela nisingeenda mbugani sio vitu vyangu kabisa!! Mimi ningekua kama bongo zozo mimi ni mtalii wa tamaduni/mila/desturi kwahiyo ningezunguka mikoa yote kutalii halafu ndo niende huko nje.. ila kwenda kuwaona Tembo hapna
 
Back
Top Bottom