Certified_
New Member
- Apr 20, 2024
- 1
- 3
Wizara hii imekuwa ni kero kubwa sana kwa Watumishi wa Umma hasa wanaofatilia vibali vyao vya uhamisho wakiwemo wale wa kutoka Taasisi mbalimbali kwenda TRA, imekua ni kasumba ya wahudumu wa ofisi ile kujibu mbovu watumishi hawa hasa wanapofika wizarani.
Mfano mtu anatokea Geita, Katavi au sehemu yoyote nje ya Dodoma kwa nia ya kujua nini tatizo kwakua ni muda umepita tangu aambiwe ombi lake linakamilishwa.Hivi karibuni na akifika pale hawampi jibu la kueleweka bila kumsikiliza mtu huyu kwa undani na kumsaidia zaidi tu ataambiwa linafanyiwa kazi.
Yes ni kweli anafaham na ndio maana anataka kujua nini kimezuilia kibali chake kwa muda mrefu; tunao watumishi kadha waliofanya interview ya TRA na wakafaulu lakini wamekuwa wakizungushwa vibali vyao miezi nenda rudi na wako katika hali mbaya ya kutokujua nini tatizo kwakuwa vibali vya watu wanaoenda Taasisi zingine zinatoka kila siku isipokuwa wao wakiuliza tatizo hawaambiwi, wadau tunaomba mpaze sauti kwa wizara hii inatesa watumishi kwa kujiona Miungu watu.
Kila mmoja ana haki ya kufanya kazi aliko qualify kwa maslahi ya taifa na yake binafsi unapozuilia uhamisho wake wewe haikusaidii maana itafika muda utaondolewa hapo kwa kuhamishwa pia au utastaafu na umeshaumiza watu kwa kutokuwapa haki zao kama inavyotakiwa ufanye. Badala yake watumishi wa Wizara hiyo wapo kuzuia na sio kuwezesha maslahi ya watumishi.