HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Ila pia nimeona wale ambao walikuwa wameshapata kazi hivi karibuni hawajachukuliwa tena na TRA.
Nadhani Yale mambo ya double placement wameanza kuyashughulikia.Naimani vingi watafanyia kazi....
November na December tunawasubiri pia Kwa placement mwezi huu asee.Ni muda Sasa ushapita.
 

Jamaa kaongea Point sana, tuishi humu kuna jamaa yangu kapata hizi Placement za TRA leo ila mzee wake yuko pale HQ ana cheo kikubwa tu. Alinambia nimepiga oral bhs kazi nimepata na nitabaki hapahapa Dar kazi kweli kapata tayari. Sometimes hata wewe fikiri uko interview na mtoto wa mkuu wa mkoa wote mnapiga Oral hivi unafikiri utatoboa?? labda Mungu akushike mkono tu.

Sisi tusio na connection tuombe sana Mungu atuguse ndugu zangu. Tuombe Mungu na pia tutafute connection. Mimi ni moja ya wahanga wa Ajira nimepitia mengi ukipitia post zangu za nyuma niligiveup kabisa kuomba kazi. Nimehudhuria interview 5 za utumishi 3 nimekwenda mpaka oral lakini mpaka leo sijawai pata kitengo. Week hii jumamosi nina oral interview nyingine ya MDA. Ninawajua wengi waliopata kazi kwa connection au kuhonga ila tatizo hawawezi kukusaidia watanyamaza kimya, ndo wabongo tulivo hatuna moyo wa kusaidiana au kuinuana.
 
daah sio poa afsa,but ipo siku tutatusua
 
Hatimae mjadala wa status umehitimishwa leo. Status ni PDF tuu.
 
Nyie wenye mawazo ya hivi ndio mnashindwaga kwa sababu ya poor mentality.Jishughulishe kujua mifumo ya PSRS na hatua za mchakato kabla ya kusema uongo na kudanganya umma unaokusoma.
 
Nyie wenye mawazo ya hivi ndio mnashindwaga kwa sababu ya poor mentality.Jishughulishe kujua mifumo ya PSRS na hatua za mchakato kabla ya kusema uongo na kudanganya umma unaokusoma.
Wale jamaa namaanisha psrs wako fair sana, kwa msailiwa aliyefanikiwa kufukia mashimo yote kipindi cha kujiandaa iwe kwa kuotea au kusoma materials yote kwa ukamilifu, ni rahisi kupenya, issue ni kubalance muda, kwa majukum ya kimaisha na maandalizi ndio changamoto ipo hapo.
 
Fact
 
Kwa interview kama hii placement ilotoka jana ya TRA vp utajua kama uko kwnye database?na ukiwa uko database kwa kada za TRA itawezekanaje upangiwe kazi sehemu zingine coz nahs kada za TRA ziko restricted kwa Tra pekee...mf customs officer au TMO
 
majina hapana yanaweza kuleta shida na migogoro hasa pale muda wa jina la msailiwa kuwepo database kuisha kabla ya nafasi kupatikana.
Lkn naunga mkono ujumbe wa post yako uliobakia.
 
Nimepata ajira ya TRA, Sina connection, sina ndugu anaefanya kazi serikalini, sina ninaemjua utumishi, sikuvujishiwa mtihani, sikujua maswali ya oral.. Nilijiandaa vizuri mengine nikamuachia mungu.. Utumishi Wapo Fair.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…