HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Jamaa wanzngua sn mpk tunaanza kutamani matapishi...hizi mambo za michakto mwaka mzima unaisha hyakubaliki na matamko ya urongo waache
#watoe hizo nafsi 1769 walizosema
 




Tukae humu.

Utumishi ni mwokozi wa watoto wa maskini wasio na connection ya mjomba pale TRA wala bamkubwa kule TCRA.

Kinachowabeba ni kua na nondo tu na kujiandaa vizuri na mtihani.

Saili zikirudi kwenye mashirika, kilio chake nyie acheni. Tujisahihishe penye mapungufu, hatuwezi kurudi tena Misri.
 
Turudi tu huko huko!
 
Hii hoja haifai kuungwa mkono hata kidogo hii, ni bora mchakato uchelewe, ila upitie PSRS.
Taasisi zikirejeshewa mamlaka zenyewe watarudia uhuni uleule wa kuwa ukoo mzima unajazana kwenye taasisi ya umma, huku wasiokuwa na Godfathers wanasota mtaani hata kama wana vigezo.

PSRS iboreshwe tu, ili iongeze ufanisi wa kazi.
 
WAACHE KUCHELEWESHA MICHAKATO WA AJIRA,HAIINGII AKILINI KAZI 1 ICHUKUE MIEZI MPKA 8 SASA WALIITANGAZA YA NINI...HAIKUBALIKI HILI SUALA
 
Kwani taasisi ikiendesha mchakato wakawepo hao utumishi kushihudia mchakto wote mpk anaptakina muajiriwa alieshinda saili hapo vipi?
 
Hii
 
Ili ujue hao taasisi wenyewe washachoka kusubili watu wapya kazini kutoka utumishi i jinsi ambavyo unakuta ofisi nzima robo mpaka nusu ya wafanyakazi ni intern na ajira za mikataba.

Tembeleeni ofisi mbalimbali mtajionea na siku hizi mpaka halmashauri unakuta wa mikataba wamejaa,hii ni impact ya jiwe miaka sita kutoajili ilihali population inayohitaji service unakuwa kwa kasi sana (angalieni takwimu za sensa)na wanaohitaji kazi pia kuongezeka pasi na kuajiliwa,sekta binafsi zilikufa sana tu japo najua kuna wakina tomaso wao watasema tu acha utumishi ndio kimbilio,tunafanya tu ubinafsi kwani ni wangapi enzi za taasisi kuajili wametoka vijijini kwetu huko hawana connection na wana kazi nzuri?

Mbona wengi tu walikuwa wanapata kazi kupitia ubest students taasisi mbalimbali(hii iliweka ushindani hadi vyuo)maana ilikuwa unakuta wanafunzi karibu 10 wote wa ufaulu wa juu walikuwa wanalamba asali.
Leo mtu ameshiba ugali anasema eti utumishi imesaidia sana ilihali imeibua ugonjwa mpya wa sonona..utaratibu wa saili popote duniani hamna usaili wa kuchukua mwaka otherwise ajira imefutwa haipo(only Tanzania)imefika muda watu mpaka tunahisi wanamhujumu Mama.

Maana website yao nadhani ndio web ya serikali inayotembelewa sana currently.

Wote wanaosema bora ajira zirudi kwenye taasisi sio kuwa wana ndugu ila wanaona umuhimu wa mtu kujua position yake mapema ili kuumia aumie maisha yaendelee kuliko mtu anakuwa na matumaini mwaka mzima afu anakuta hayupo anaambiwa kuna kanzidata nayo anasubiti mwaka mzima then napo anakuta hayupo, mtu wa namna hii ni umeshampotezea muda na kuharibu mindset yake kwa asilimia kubwa.

Hili neno watoto wa masikini sisi ndio limetuchelewesha miaka sita nyuma kwa kupeana matumaini...hiko utumishi kwenyewe mm siamini kama kama mnavyodai fair ipo hata huko rafu zinachezwa sana tu kila mmoja anajua rafu anavyoicheza hadi alambe asali ila kamwe hawezi kukuambia atakuambia ni Mungu tu na kujiandaa.

Kwa hili ilipaswa tuungane wote tujue shida ni nini au marks za oral nazo ni mchakato unafanyika maana hii chelewa chelewa inaleta maswali.

Anayebisha aende akaangalie yale majina ya NAOT auditors then aende akaangalie majina ya staff wengi wa NAOT aje abishe kwa hoja sio kutetea tu vitu ambavyo hatujui.
 

Aisee, sikulijua hili mkuu ingawa naliweka kwenye nadharia.

Tuwe na subira hata kama inafikia wakati subira inakuwa ngumu kuivumilia, siku ikifika utasahau haya yote
 
NI kweli uncle 🙏, marks za oral interview Zina zengwe sana ,na Ndio maana mkeka wa database unachelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…