HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Taja taasisi na namba za simu au unaogopa?
 
kinacho umiza utumishi wanatangaza nafasi mpya zenye waliofaulu saili za nyuma badala wawape waliopo database.

Sekretarieti ya Ajira

Sent from my SM-N900 using JamiiForums mobile app
Si mumesema hamtaki kupangiwa sehemu ambazo hamkuzifanyia sahili?

Kama hujaona hiyo comment, fuatilia comments za jana hadi leo utaona hilo wazo.

NB: Kama kweli mnataka mabadiliko ya kiutendaji huko PSRS, jaribuni kuwa na msimamo na wala si leo mtu anasema hiki, kesho akasema kingine kinyume na alichokisema mwanzo.

Tuliopata placement, tukiwaasa mvumilie mnatuona sisi ni mawakala wa PSRS, nimebaki kusoma comment zenu sana badala ya kuchangia na nachangia pale inapobidili tu ili mpate uwanja mpana wa kuwasema PSRS.
 
Mkuu, hio comment mimi pia niliisoma huko juu. Nikajisemea kumbe tupo tofauti tofauti humu kwenye suala la kupata ajira.
Ila kwa mimi na nafsi yangu, hata nipangiwe kituo cha kazi huko ndani wanapokataa wengine, I will be ready to go. Tena, I wish itokee kwenye PDF ninayoisubiri.
 
sheria na kanuni yao inasema hawaruhusiwi kutangaza nafasi mpya kama kwa kada hiyo inayo waliofaulu saili za nyuma na kuwepo Database. ila taasisi zikipeleka vibali basi watawachukua wale waliopo database na kuwapangia kazi kwa kada ile na nafasi zilizoletwa na taasisis husika.

mfano kuna tangazo walitoa tarehe 17/3/2023. tanzania railway cooperation(TRC) ambayo ni taasisi ya serekali.

kwenye hilo tangazo tuchukulie MFANO kada ya " medical laboratory technology" ambayo nyuma ilifanya usaili JKCI pamoja na AICC. naamini kwa kada iyo kwa wale wote waliofanya zile saili za nyuma basi kuna ambao walifaulu wakapata placement wengine walifaulu pia ila hawakupata placement kulingana na ufinyu wa nafasi ila wakawekwa database. maana haiwezekani eti wote watakuwa walifeli wakosekane ata wachache wa database.

sasa kuna haja gani ya kutangaza tena nafasi mpya kwa kada hiyo na kuwaita tena kwenye usaili wakati kuna ambao walifaulu na wapo database sasa kwanini wasipangiwe kazi kwa hiyo taasisi iliyoleta kibali. na ingesaidia kupunguza garama upande wa serekali na upande wa wasailiwa ambao wanaomba tena wakati walifaulu saili hizo za nyuma

Hapo ndipo tunaona pengine utumishi wanawatu wao wamewaanda ili wawape izo nafasi.

Sent from my SM-N900 using JamiiForums mobile app
 
Mchakato wote wa ajira huwa unahusisha PSRS na mwajiri, mwajiri ndio anasema anachokitaka halafu PSRS inamfanyia.

Sasa kama mwajiri hataki watu wa database hapo lazima nafasi itangazwe.
 
khee umegeuka motivational speaker tayari hahaha
 
Mchakato wote wa ajira huwa unahusisha PSRS na mwajiri, mwajiri ndio anasema anachokitaka halafu PSRS inamfanyia.

Sasa kama mwajiri hataki watu wa database hapo lazima nafasi itangazwe.
sasa kuna haja gani yakuwa na PSRS kama taasisi ndio inamamlaka kuliko wao?

na PSRS itaitaje watu waliofaulu usaili kwenye usaili mpya tena. Hichi ndo kitu waziri jenista alikilaani bungeni na kusema ataajiri watu 1760 kutoka database ili kuepusha kuwarudisha rudisha watu waliofaulu usaili kwenye saili zingine mpya.

Sekretarieti ya Ajira fanyeni kazi zenu kwa kufuata kanuni zinazowaongoza sasa nyie wenyewe mnavunja kanuni zenu ni bora muachie tu taasisi zifanye saili zenyewe kama zenyewe ndio zinamamlaka kuliko nyie. au raisi samia awaondoe tu maana mnakera

Sent from my SM-N900 using JamiiForums mobile app
 
Mchakato wote wa ajira huwa unahusisha PSRS na mwajiri, mwajiri ndio anasema anachokitaka halafu PSRS inamfanyia.

Sasa kama mwajiri hataki watu wa database hapo lazima nafasi itangazwe.
basi psrs ni taasisi hewa yani taasisi wako juu yao
yani mmepata ajira mmekuwa kama polepole alivyopataga asali haha
 
Inaweza ikawa ni mtu wa kujifunza kweli, lakini katika hili, pamoja na kupata kwako taarifa hakujasaidia lolote katika uzi huu, uzi unahoji nini kinachopeleka kuchelewa placement badaada ya oral, limeongezeka lingine hapa, nini kinakwamisha kutolewa kwa pdf la database ilhali deadline imeshapita toka waziri atangaze.

Ingekua una lengo lankutia moyo watu humu, ilifaa, utueleze hapa, jamani kwa maaelezo niliyopata toka psrs/moja wa watumishi psrs ni kuwa, placement huchelewa kwa sababu kadhaa, moja,.... Pili,.... Tatu... Hapo ungekua umesaidia wengi humu, sio kwa hoja zako za kipindi hiki, watu wakihoji, jibu kuweni wavumilivu, mara watu wajiandae vya kutosha, mara wtau watenge muda kujisomea yaani iwe ratiba kabisa kama walevi walivyojiwekea ratiba kupata vitu vyao.

Kuna mengi watu wanahitajibkujifunza kupitia uzi huu, dodoso la kinachoendelea baada ya oral, kinachopelekea kucheleweshwa sana placement, na sasa limeongezeka, nini ni kikwazo dhidi ya pdf la database.

Hizi mambo za kukata tamaa sidhani kama zina uzito kutolewa ma mtu kama wewe, ndio maama kila sahili watu wanahudhuria pamoja nankuwa wanakandwa, nasisitiza, umesema wewe ni mtu wa kujifunza, na ukaitumia fursa ya kukutana na psrs kuzungumza nao, na wamekueleza mengi, ni wasaa sasa kutueleza hapa nasi tujifunze na kufaham hasa kinachopelekea kuchelewa kwa placement.
 
Mkuu mengine ni Siri,sio kila jambo la kuweka hadharani,Kikubwa tu tutimize ya kwetu,Tumuombe Mungu na tuendelee kusubiri.Kama wewe ulivyosema ya kuwa mwaka huu utaleta Ushuhuda,basi tuendelee kupambana Mkuu
 
Mkuu mengine ni Siri,sio kila jambo la kuweka hadharani,Kikubwa tu tutimize ya kwetu,Tumuombe Mungu na tuendelee kusubiri.Kama wewe ulivyosema ya kuwa mwaka huu utaleta Ushuhuda,basi tuendelee kupambana Mkuu
Acha masihara wewe, mambo ya siri wakueleze kirahisi tu kwa kua umeenda kufata barua ya ajira. Hivi unajua maana ya siri mkuu? Yaani mwajiriwa wa taasisi/taasisi iwe tayari kukueleza taarifa katika mazungumzo tu ya kawaida, halafu, useme taarifa hiyo ni siri, hilo halipo.
 
Tunatofautiana upeo na uwezo wa kuchakata mambo kun watu humu wanaongea vitu hawafikirii mana hatua ya kwanza kupata mrija mtu hajavuka anawaza yapili anachagua pakwenda.. Kikubwa tupambane tuingie kwenye system kwanza..alafu sio vyema mtu akitoa mawazo yake kwa kuwa amepta asali uku mnaanza kumu attack kuwa ana defend utumishi haijakaa sawa ni mawazo ya mtu tuwe flexible tusikaze vichwa tukae position ya kujifunza na kuthamin michango ya wanaochangia
 
Huu ujumbe umetulia sana.....
 
Wako bize kupanga watu wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…