HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
dah kumbe na wewe ni mkongwe kama mimi, umenikumbusha enzi za DUCE.
 
yaah afsa ni kweli japo inauma sna, na ukumbuke nawe ulitoweka ghafla baada ya kukosa placement mpaka tukaanza kukuulizia ukowapi balozi.

ukarejea ghafla na ID mpya baada ya kutusua kupitia database ama naongea uongo mkuu?
Nakubali mkuu, na ndio maana nikasema hizi nyakati sote humu tumepitia naamini mambo mazuri yanakuja ni suala la muda tu, mm mwenyewe mpaka nilipoteaga kabisa humu sikutaka kuingia tena baada ya kufanya oral nyingi bila kupata placement lkn muda wangu ulipofika basi ndio ulikuwa wakati sahihi, nisingeweza kulazimisha huenda sikupangiwa kule.
Tuweke hoja tu za kujenga ili tuboreshe lakini tusilalamike sana mpaka tukavuka mipaka, naamini baada ya muda wote mtakuwa mmepata, ni kheri ya kwetu sisi ambao tumepata na still tumo humu, kuna wengine walilalamika na baada ya kupata walipotea na hata wengineo humu wakipata watapotea na ndio huwezi kumlazimisha mtu, tujengane, tuweke hoja za msingi na tukosoe kisomi wahusika wataona tu na kuweka sawa.
 
Usiamini status hakuna anayejua ukwel hapa Siri imabaki kwao uko psrs kikubwa amin katika pdf
 
Samahani mkuu we ndo wizy

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
sahihi mkuu
 
Me nafikiri utumishi waamie kwenye uptitude test. Kutoa madesa ya darasani naona si sawa sababu kuna watu wamemaliza miaka 5 nyuma tayari wanamajukumu kukumbuka waliyosoma miaka 3 ya chuo ni ngumu sana.

Au wawafikirie graduates wa nyuma ambao oral watapata pass wawape kazi, kuna watu wanapigika sana kitaaa. Unakuta aliyemaliza 2014 oral ana 60 aliyemaliza 2021 ana 80 utumishi wanampa wa 2021, hivi hawa uwezo wa kufikiri utakua sawa?? Its not fair ukikumbuka ajira zilikua za shida kipindi cha magufuli. Utumishi walifikirie hili sana.

Nilipata tetesi utumishi kuanza kuwapa kipaumbele wenye age kubwa kama ni kweli bhs watakua wamefanya jambo jema.
 
Wanawapa kipaumbele wenye umri mkubwa kama wamelingana marks na mwenye umri mdogo...


Kwa mujibu wa muongozo wao, order ipo hivi:

  • Mwenye ulemavu
  • Mwenye umri mkubwa
  • Mwanamke

Ukilingana marks na hawa watu, umeliwa kichwa
 
Kwa sasa huwezi kuongea kwani una asali na chakula mdomoni!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…