HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Wadau wa halmashaurii hawajaishaa tuu ?[emoji28] maana naona watu wa taasisi tumeekwa pending sjui mpk waishe wa halmashaurii[emoji28][emoji2357]
PSRS Wanaviporo vingi vya nyuma japo wanashindwa kusema tena wanajitahidi sana unaweza kuta wanabarua nyingi sanaa za watu tatizo likawa kwa maboss wao Utumishi..... Utumishi wanachelewa kutoa mrejesho wa vibali vya kuajiri watu ila Bungeni wanajinadi wametoa 10,000+ ... Hofu ya Mungu hawana kabisa Utumishi ila vijana tusikate Tamaa ni swala la uvumilivu tu kama Mungu amekupangia kupata utapata tu...cha msingi usiache Kumlilia mbele zake
Hongeren mliotoka kwenye Mkeka wa jana Mkawe Watumishi wema kwa Wananchi...
 
Sawa WAKALA Jr
 
Tatizo kubwa ni kwamba hiyo DATABASE haiko wazi!! Hakuna anayepewa taarifa kuwa alifaulu usaili na jina lake liko kwenye database!! Hiyo Database ni KICHAKA cha upigaji! Napendekezwa hiyo database iwekwe wazi!!
 
Ushauri wako mzuri sana!! Kuna dogo alifanya interview 4, moja aliikacha yaani aliitwa kwenye usaili mara 5 na kuhudhuria 4. Kila usaili alikuwa anatumia kama laki moja na nusu kwa ajili ya usafiri toka huko mikoani na malazi kwenda Dodoma mara 2, Moshi mara moja, na morogoro mara moja, aliikacha 1 ya dodoma. Ule usaili wake wa 4 huko dodoma ndo alifanikisha na ameshaitwa mwezi huu. Fikiria gharama hiyo yote wakati huna ajira utaimudu hadi lini? Ndio maana siku hizi wanaohudhuria usaili hasa ule wa writte ni kama nusu tu ya walioitwa! Wazazi wanafika mahali wanashindwa kusapoti usaili wa vijana wao!!
 
Wanatakiwa wafanye nini sasa mbona tunakua hatuna jema kabisa wakiitisha sahili mpya tunakosoa na wakitaka kuchukua watu wa database ili wakiisha ndio waitishe sahili mpya bado tunakosoa ama kweli bado tuna safari ndefu sna
Usichojua ni kwamba kanzidata/database ni kichaka cha upigaji!! Ndio maana hakiko wazi wala hakuna ajuaye kwa uhakika kuwa ni kina nani wako kwenye database. Na ni utaratibu upi unatumika kuchomoa hao walioko kwenye database. Basi watoe mkeka wa watu wote walioko huko database ikionesha walivyopangwa foleni ya kuitwa!
 
Nakuunga mkono na naomba wote tuunge mkono mawazo yako!! Hii database ni kichaka cha kupitisha watu kwa mlango wa nyuma!! Ndio maana hii database haijawahi kuwekwa wazi wala hakuna ajuaye kwa uhakika kuwa jina lake liko kwenye database!! Hii ni kwa sababu marks za oral interview huwa haziwekwi wazi kwa hiyo usipopata placement inachukuliwa kuwa ulifeli. Wanapoita watu kwenye ajira huwa wanasema hivi:
Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.

Kwa hiyo usipoitwa ni aidha ulifaulu na hukupata nafasi au hukufaulu!! Kwa nini wasingekuwa wazi ni kina nani walifaulu lakini nhawakupata nafasi ili waendelee kusubiri kwa matumaini kwa uhakika wa kuwa kwenye hiyo database? Narudia hayo mambo ya database yafutwe maana ni mlango wa nyuma huo!! Kila nafasi igombaniwe kwa upya ili kutoa fursa kwa wote sawa! Vinginevyo kuna watu watakuwa wanapachikwa kwenye hiyo database ya siri hata hawakuwahi kufaulu au hata kufanya usaili wowote!!
 
Hausemi kweli!! Utajuaje kuwa umefaulu mtihani wa oral na umekosa tu nafasi waki marksi za oral huwa haziwekwi wazi? Hakuna ambaye ana uhakika kuwa jina lake liko kwenye database maana psrs huwa haitoi mkeka wa marksi za oral wala huwa haitoi mkeka wa hiyo database!! Hiyo database ni mlango wa nyuma wa kupitishia WATEULE wachache!! Huu utaratibu wa gizani wa database ufutwe mara moja!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…