HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Hongera sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikuambie kitu: Unapojisikia kukata tamaa ujue muujiza wako uko karibu sana!! Jitie nguvu, jipe moyo na uendelee kuomba nafasi kila zinapotokea na kufanya usaili. Ni kweli zinamaliza pesa lakini hayo ndiyo matumizi sahihi ya pesa!! Kuna watu ninaowajua walikuwa wamekata tamaa sana baada ya kufanya saili kadhaa bila mafanikio. Tunapozungumza leo tayari walisharamba asali na wako kazini tayari.
 
MD yupi???? Wa nchi gani???? Labda NGOs kwa hapa bongo ilaa Daktari baada ya makato hafiki hata milion.
Unasema kweli kabisa!! Ma-MD wakipita hapa wanashangaa sana!! Ni kweli kuna tofauti ya viwango vya ma-MD wale wanaofanya moja kwa moja serikalini na wale wanaofanya kwenye taasisi za sertikali. Lakini kwa MD anayeanza kazi hakuna anayetoboa 2M gross salary. Wa kwenye taasisi kama vile Muhimbili hospital, MOI nk wako juu kidogo kuliko walioko LGA. Wale wa LGA baada ya makato milioni haipati. Wale wa kwenye taasisi baada ya makato anapata milioni na ushee kidogo!.
 
Wakati wa Mungu ni wakati sahihi sana kikubwa tusikate tamaa kuapply na kuattend kwenye interviews na kufanya maombi piah, kila mtu atapata kwa wakati wake.
Nashukuru Mungu nimebahatika kupata kazi kwenye pdf ya jana hakika Mungu ni mwema[emoji119].
Hongera sana na ukawe mtumishi mwema. Endelea kuwaombea waliobaki nao warambe asali.
 
Sa kwanini walimu wanalalamika sana maisha magumu kuliko hao MaHR, na wengineo walioko Halmashauri?
Hao wengine wako jikoni wakati mwalimu yuko Dinning.
Nakupa mifano miwili :

1. Afisa hesabu wa Halmashauri anaesimamia Zahanati na hospital madokezo yote ya Hela na miradi mbali mbali lazima yapite kwake hapa lazima adake chochote akikusanya Zahanati zote sio haba

2. Procurement hawa ndio hawaendi mbinguni kabisa Kila mradi wa Halmashauri lazima wale. Hawa wanaenda sambamba na wahandisi. Mmoja anakagua utaalamu wa vifaa mwingine anakagua bei. Ukisikia Halmashauri imejenga soko Kwa milioni 800 basi ujue gharama halisi ni milioni 450-500, hizi nyingine mgao umetembea bila kumsahau pacha wao Afisa hesabu na mchumi.
Pia Hawa wa Halmashauri makao makuu wana OT wanajilipa.
Mwalimu Hana kitu chochote mkavu kama mkaa Hadi mwisho wa mwaka apate fursa ya mitihani
 
Vipi kuhusu ma afisa wa idara ya ukaguzi wa ndani Halmashauri nao wapoje upande wa posho?
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…