HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Hapana Psrs ndio kikwazo...mwajiri anahitaji manpower.
 
Huu ujumbe kwa WAKWEPA KODI ingekua vizuri ungewaandikia MIJIZI YA SERIKALINI ambayo kila siku tuona kwenye ripoti ya CAG
 
Hapana Psrs ndio kikwazo...mwajiri anahitaji manpower.
Ni kweli mwajiri anahitaji manpower ndiyo maana aliiomba! Lakini japokuwa iko kwenye mpango lakini hajawezeshwa bado kuwapokea!! Atawapokea kwa kadri anavyowezeshwa!! Vinginevyo mwajiri ndiyo angeilalamikia PSRS!! Hivi ni mwajiri gani atamvumilia wakala (PSRS) kutumia mwaka mzima ndo atekeleze jukumu alilopewa? Kama inmgekuwa hivyo waajiri wangeshamlalamikia PSRS siku nyingi!!
 
Inawezekana kabisa wanamlalamikia kakini mm na wewe hatujui.
 
Unamaanisha katinya psrs na mwajiri nani mwenye nguvu???
PSRS unatakiwa ujue wapo chini ya Rais.
Ni bora wasitangaze anira kabisa kuliko wanachofanya,awamu ya tano hawakuajili kwa winginlakini chache zilifanyika kwa wakati,au shida ya hela imeanza juwa miaka ya karibuni tu,mbona kipindi cha nyuma haikuwepo hii kitu??
Kuna uzembe upo mahali na sio kuutetea tu ambapo hakuna maana.
 
kuna viashilia vingi vinavyofanya niamini psrs wanazingua tena sana. Japo idea ya wao kusimamia haya mambo ni nzuri lkn baadh ya taratibu zao ( hasa kuchelewesha placement na kurefusha muda kwenye mambo yao ) zina madhara mengi kiasi ambacho naona ni bora tyuu sasa wasingekuwepo iwe kama zamani watu wabebane potelea mbali.

Kwa nini nasema hivi. ?

Serikali HAINA UWEZO wa kuajili vijana wote, kisaikolojia ninaamini hivyo,. Sasa kwa nini psrs inaweka watu kwenye tension kwa muda mrefu. Ankoo ujue hali niliyonayo mimi kwa sasa sijui kwa wengine nimeshindwa kufanya mambo yangu kwa ufanisi kama mwanzo, nina shauku ambayo imegeuka kuwa huzuni kwa takribani zaidi ya mwaka sasa.
Na ikiwa wewe unachosema ni kweli kwamba taasisi ndo zenye shida kwa nn psrs wasitoe placement mapema. Coz kusubirisha wachache ambao wanajua wamepata kazi ni bora japo nao watakuwa matamanio makubwa kuanza kazi ila maumivu yake si sawa na haya, kuliko kuumiza kundi kubwa la watu ambao wengi wao huna mpango nao yaani wamefeli na hutakuwa nao.

Hii sio fear hata kidogo ankoo hili ni jambo baya sana na PSRS wanahusika 99.9999%.( kadiriaa kiwango kimoja chadesimali upate asilimia/percentage kamili Za uzinguaji wao).
 
Ila kwa kwel inaumiza sana kwanini wasiwe wanatoa majina yote kwa mkupuo mmoja, au labda kuna sababu ya Msingi sana inayowafanya watoe nusu nusu Ivo, nadhan kuna tatizo hapo
 
Tukubaliane kutokukubaliana kwa amani: Siyo suala la nani ana nguvu bali ni suala la nani ana majukumu gani, na wote wanatekeleza majukumu yao chini ya Rais, ambaye ndiye mwajiri mkuu wa watumishi wote wa umma kwa niaba ya watanzania. Na Rais mwenyewe akiwa ni mwajiriwa wa watanzania, waliyemwajiri kwa kura zao, ili awatumikie kwa mujibu wa katiba.

Kama ugali haujaiva, haujaiva tu, huwezi kulazimisha ukaribishwe mezani!! Na kama mtu akikukaribisha mezani wakati ugali bado unaandaliwa, utasubiri sana hapo mezani hadi kero!! Ni rahisi sana kupata matokeo ya oral interview kuliko ya written, kwanza oral interview inahusisha wachache!! Kama kila kitu kingekuwa tayari, placement ingekuwa inafanyika kwa haraka zaidi kuliko matokeo ya written yanavyotoka!!

Ukiona placement inachelewa ujue kuna mambo yanatakiwa kuwekwa sawa!
 
Reactions: Grj

msome mzee [mention]mbingunikwetu [/mention] katika hali ya utulivu na utapata kitu. Ni mkongwe kwenye utumishi na ana uzoefu mkubwa katika masuala ya rasilimali watu. Hanufaiki chochote kuwatetea PSRS.
 
Braza ukubali ukatae PSRS ni tatizo kwa afya ya akili ya vijana wasaka ajira,mchangiaji hapo juu ametolea mfano yeye binafsi kabisa,unapofanya oral huwa tunajiasses kabisa ulichojibu kama kipo sawa kwa vile maswali yao huwa ni clear yana majibu yanayofahamika sio ya uelewa kwamba utafikiria uuungeunge,sasa watu wanapojiasses na kuona kuwa alijibu sahihi na majibu yake humpi na husemi tatizo nini ndio shida inapokuwa kubwa,.tungekuwa tunajenga hoja kwa pamoja kuwadai matokeo ingekuwa ni vizuri zaidi.

Bro hali hii inaumiza sana hujui tu,kwa nini mambo mengine yakitokea wanakimbilia kueleza umma kuwa shida ni kitu flan lkn hili linalihusu vijana wanakaa kimya? PSRS ina afisa habari wake kwa nn haujulishi umma kuwa wao sio shida??(umeme ulikatika Taifa pale na bungeni dakika chache tu kila mmoja akawa anatoa press release kusema sio muhusika)

Kama ndugu zetu wanaripoti vituoni na wanaambiwa shida ni psrs ndio inachelewesha kwa nn tusiamini ilihali wao psrs wamelala usingizi hawana muda na sisi,barua zinaandikwa mwezi wa pili mtu anaitwa kazini mwezi wa nne kisa wa kusaini alikuwa bize napo tuseme tatizo muajiri?

Serikali inakuja inasema mwaka flan wa fedha tumeajiri watu 50k ambao hatujui waliajiriwa lini na wapi maana ukipitia placement za tamisemi halmashauri zote na wao psrs idadi haifiki,sasa kuna mantiki gani ya kuendelea kutangaza ajira ilihali fungu la kulipa halipo ila mwisho wa mwaka wawakikishi wanapiga makofi bungeni na kupitisha mishahara mipya kwa wafanyakazi wapya ambao mnasema hela hazipo ila tipoti ikija kuna ubadhilifu wa fedha.

Tukubali tu PSRS ndio shida kwa sisi wasaka asali kwa usiri wao usio na msingi, sometimes watu tunasema bora taasisi waajairi sio kuwa tuna ndugu au connection lakn bora nikose nijue nimekosa maisha yaendelee lkn sio kumaliza bando kuchungulia website kila siku.
 
Na ikiwa wewe unachosema ni kweli kwamba taasisi ndo zenye shida kwa nn h psrs wasitoe placement mapema. Coz kusubirisha wachache ambao wanajua wamepata kazi ni bora
Hilo linaweza kufanyika ila pia watalalamikiwa sana na hawataeleweka kama wanavyolalamikiwa sasa.

Tuchukue mfano wa posts za MDA&LGA ambazo zilitangazwa May 2022. Baada ya mwezi mmoja wangeitisha usaili yaani June 2022 na June hiyo hiyo 2022 wangetoa placement. Lakini ujue kuwa ajira hizo zilikuwa zimewekwa kwenye bajet ya 2022/2023 ambazo pesa yake bado haijakusanywa hata shilingi moja maana mwaka wa fedha huanza Julai mosi!! Halafu wangelazimika kusubiri hadi April 2023 ambapo ndiyo MDA&LDA wameanza kupata hilo fungu walilotengewa kwenye bajeti baada ya kuwa limepatikana!! Je unafikiri kusingekuwa na malalamiko?

Kuna watu hawajui kama serikali inaweza kuwa haijapata pesa ilizotarajia. kwa hao ni vigumu sana kuelewa! Narudia tena, serikali yoyote haina ujanja wa kupata pesa zaidi ya makusanyo ya kodi, mikopo, na gawio mahali ambapo imewekeza. Lakini chanzo kikuu ni kodi!! Kama kodi ingekuwa inakusanywa kwa kasi iliyotarajiwa matatizo haya yangepungua sana.

Ni kweli kabisa wizara nyingi kama siyo zote huwa hazifanikiwi kupewa pesa yote iliyoidhinishiwa kwenye bajeti. Ikitokea hivyo mambo hutekelezwa kwa vipaumbele, na mambo mengine husubirishwa!!
 
Kwanini watoe tangazo May 2022 huku wakijua mwaka wa fedha ni wa 2023?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…