HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
PSRS wanatangaza kwa niaba ya waajiri!! Hawatangazi wao kama wao!! Cheki hapa tangazo la PSRS ambavyo huwa linasomeka!!

On behalf of Dar es Salaam University College of Education (DUCE), Institute of AdultEducation (IAE), University of Dar es salaam (UDSM), Livestock Training Agency (LITA),Tanzania Veterinary Laboratory Agency (TVLA) and Tanzania Fisheries ResearchInstitute (TAFIRI) Public Service Recruitment Secretariat (PSRS) invites dynamic ...................

Anayeamua kutangaza kazi siyo PSRS bali ni mwajiri!! Kwa hiyo kama kuna lawama kwa kutangaza ajira ambazo zilishafanyiwa usaili na taasisi zingine, lawama hizo zielekezwe kwa waajiri hao, na si kwa PSRS ambaye hutangaza kwa niaba (On behalf) ya waajiri hao!!. Sisi wote tunajua maana ya kufanya kitu kwa niaba ya mtu fulani!! Waswahili husema "mjumbe hauawi", lakini kuna watu wanajitoa ufahamu na kutaka kumwua mjumbe!! Kwa maneno mengine PSRS ni mshenga tu!! mwoaji ni mwajiri!!
 
We nae una misiasa kibao asee
 
Kwa hiyo wewe unaona kama nafasi ni moja na waliofanya oral ni watatu kwa hiyo ni lazima afaulu mtu mmoja tu!! kwamba hakuna uwezekano wa kufaulu wawili au wakafaulu wote watatu lakini wakazidiana marks!! Kama ni kweli unadhani hivyo basi ni niseme "UKO SAHIHI" na tuishie hapo!!
 
Sina muda wa kujibizana na wakala wa psrs.
Mimi nimesoma Sheria na kanuni za psrs naelewa kila kitu na haipo hivyo kama unavyosema.
Zile taasis zilizokasimiwa kuajiri wenyewe psrs wakahusishwa kama third party for fairness n equity ndicho unachozungumzia wewe
Kwa hiyo usije hapa kupotosha watu na kujiona unaelewa kila kitu wakati watu tumeanza na huu Uzi na kanuni zao zote zilitumwa huku tukawa tunazichambua
 
Hata wakifaulu wote mbona written wanaongeza pass mark wale best wakapata nafasi
 
Siyo siasa ni ukweli ulivyo na nimenukuu mojawapo ya tangazo la PSRS na wewe unaweza ukajisomea mwenyewe kila tangazo!!
Hapana unawapotosha watu psrs wapo kwa niaba ya serikali kussuaply watumishi na sio kwamba kwa kuandika kwa niaba ya ndio taasisi inajiamulia hapo big no
Kama ulifatilia zile ajira za tra had rais akawa anawalaumu psrs ndio utaelewa wao ndio wenye full authority hivyo taasisi haiwezi kuwa above psrs
 
Umeongea ukweli jamaa anapostosha sana
 
Japo mm mweny
Japo, mm mwenyewe ni muhanga wa placement lakn mwamba namkubali kwa nondo anazoshusha hapa!!
 
Basi tuseme PSRS ina uwezo wa kutoa placement isipokuwa inadengua tu!!. Na itoe placement kwa wote waliofanya usaili fasta!! Isipofanya hivyo ndani ya siku tatu, serikali iifute mara moja!! Na kwa nini serikali haijaichukulia hatua muda wote huu wakati malalamiko ni kibao?
 
Kwa hiyo kwa mujibu wa maelezo yako, hata nafasi za MDA & LGA ni kwamba MDA na LGA walikasimiwa kuajiri wengine, maana pia tangazo la ajira hizo toka PSRS linasema "Kwa niaba ya...". Lakini ukweli kila mmoja anaujua kwamba MDA & LGA hawajakasimiwa kuajiri wenyewe!! Tangazo lake hili hapa:

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Makatibu Wakuu wa Wizara,Watendaji Wakuu wa Idara Zinazojitegemea, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi waHalmashauri za Jiji/Manispaa/Miji na Wilaya anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzaniawenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi Elfu mbili na hamsini na saba (2057) kama ilivyoainishwakatika tangazo hili.

Nawatakia wote mafanikio, na kuna siku itabaki ni historia baada ya kuramba asali. Lakini tusiufumbie macho ukweli, maana mwisho wa siku haitatusaidia!

Kumlalamikia mshenga atekelezaye maagizo na maelekezo ya mwoaji tutakuwa hatumtendei haki!! Hii haina maana kuwa PSRS hawana mapungufu, la hata kidogo, hakuna taasisi isiyokuwa na mapungufu ili maadamu inaendeshwa na watu wala si malaika!!
 
Na Ndio maana tunataka Taasisi na mashirika yafanye. Saili wenyewe
 

Well said!!



[emoji120]ipo siku Mungu atatupa Baraka ya kupata kazi, na tutashuhudia na kutoa shukrani, tuzidi kumuomba Mungu.
 
Tatizo lako unapotosha LGA MDA hazijakasimiwa ndio lakin kitendo cha kutaja kwa niaba ya taasisi a na b lengo ni kuwajulisha wasahiliwa taasis anayoomba na ambayo yupo tayari kufanya kazi na si vinginevyo kama wewe unavyopotosha hapa.
Kwanini wanataja kwa niaba ya taasisi Fulani lengo ni anayeomba kazi kupata full details huwezi toa tangazo e.g psrs tunahitaji wahasibu( ili Hali hao wahasibu wanaitajika veta) hiyo haiwezekani kwa sababu lengo la psrs ni recruitment so lazima wataje taasisi husika na sio kama unavyopotosha umma
Pia kumbuka kila applicant ana choice yake mfano mm ni mchumi lakini sipo tayar kufanya kazi halmashaur au taasis Fulani
Ndio maana wanataja kwa lengo la kuepuka usumbufu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…