HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika


PSRS wanalipa mishahara??
 
Basi acha mawenge mzee, unaonekana una mchecheto sana. Fanya oral potezea wakati wako ukifika utafikiwa tu.
Sidhani kama ipo sawa kwa maelezo yako eti wakat wako utafika. Yani sijui mnaelewa hv mfano nimekuja hospital naumwa ukanipima nikakutwa mgonjwa then utasema haya rudi nyumban unaumwa wakat wako ukifika utapona. Ndicho psrs wanachofanya sasa si bora kama taratibu hazijakamilika wasubiri ziwe sawa ili zoezi liende sambamba.
Vijana tunateseka na kupotezewa muda
 
PSRS wanalipa mishahara??
Psrs ndio serikali yenyewe ndio kazi yao hiyo sasa kinachowashinda kutoa placement taasisi ibaki na taratibu zingine ni nini? Kwani jina likitoka psrs ndio mshahara unaingia big no unaripoti kwa muajiri na taratibu zingine zitafuata. Hivyo kwa mantiki hiyo psrs hawana excuse ni bora wasifanye mchakato wa ajira hadi utaratibu uwe sawa.
 
Hivi issue ya umri , utumishi huwa wana uzingatia ? Yaaani mfani una miaka 30 point regardless ya mwaka wa kuhitimu ?
Kwenye mikando hakuna kigezo cha umri (Ii maadam umri usizidi miaka 45) wala mwaka wa kuhitimu!! Kule wanakofanya selection bila mikando (ualimu na afya through TAMISEMI), huko ndiko huzingatia mwaka wa kuhitimu na umri mnapokuwa mnagombania nafasi.
 
Kwenye mikando hakuna kigezo cha umri (Ii maadam umri usizidi miaka 45) wala mwaka wa kuhitimu!! Kule wanakofanya selection bila mikando (ualimu na afya through TAMISEMI), huko ndiko huzingatia mwaka wa kuhitimu na umri mnapokuwa mnagombania nafasi.
Kigezo cha umri kipo ukisoma kanuni zinasema wazi mkifungana marks wata consider umri,Jinsia na Ulemavu.
 
Wasaka miriji ya asali Askari mimi placement zinaathiri harakati zangu zingine na maisha yangu kwa sasa nimefikisha mwezi wa saba na siku 5 tangia nianze kusubiri placement .[emoji24]

Kuwa mvumilivu, niliomba ajira mwezi wa sita , interview nikafanya mwezi wa 11 , placement nikapata mwezi wa tano baada ya mwaka kupinduka, ajira rasmi nikaanza mwezi wa sita.
 
Kwani we unacholalamikia ni nini au unataka PSRS ifanye nini ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…