HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Hongera sana Mkuu
 
Ni wapi?

Sent from my Infinix X6816 using JamiiForums mobile app
 
Hongera sana ukawe mtumishi mwema
 
Hongera Mkuu
 
Kitenge kwa sasa hayupo PSRS sijajua kama atakua kastafu au katolewa, ukiangalia kwenye profile kuna moja ya picha utakuta wameandika watumishi wa Sekretariati ya ajira wakiwa na "ALIEKUA" katibu wa sekretariati ambae ni kitenge.
Chochote kinawezekana!! Lakini sidhani kama Kitenge atakuwa amefikisha umri wa kustaafu!!. Kama angekuwa amestaafu kwa nafasi yake asingestaafu kimyakimya. Lazima kwenye tovuti ya PSRS wangeonesha kumuaga kwa heshima! Tukumbuke Kitenge alikuwa na msimamo sana dhidi ya vimemo! alikuwa haingiliki kirahisi! Alikuwa kikwazo sana kwa wanaopenda kutumia nafasi zao kushinikiza ajira kwa watu wao!! Bila shaka walikuwa wanamlia timing tu!! Kuondolewa kimyakimya inafikirisha sana!! Inaonekana hakuna sababu ya msingi ambayo unaweza kuitumia kumtumbua!! Hiki kimya kuhusu alivyoondoka kinatisha! Wahenga walisema kimya kingi kina mshindo mkuu, ngoja tuone!!! Ni mawazo tu, I may be wrong anyway!!
 
Hongera , Status kwenye profile yako app na web zinasomaje ?
 
Mkuu na wewe ni miongoni mwa wale barua zao za tangu mweI wa nne maana kuna mtu tulifanya nae mwezi wa pili kakuta barua ya mwezi wa nne mpaka nikasema inaonekana mzee alikuwa mgumu sana kusain barua
 
cc.

CC. Mbinguninikwetu.
Hapa kuna uwezekano mkubwa PSRS ndio wamefanya makosa kwa bahati mbaya!! Ujue PSRS wanafanyisha usaili na placement kwa niaba ya mwajiri kwenye utumishi wa umma!! Kwa hiyo lazima wapeleke waajiriwa kama mwajiri alivyohitaji na si vinginevyo!! Kama mwajiri alihitaji mmoja na kuna ushahidi kuwa alihitaji mmoja huwezi ukampa wawili akawapokea wote, hana bajeti hiyo!!

Ila huyo aliyepatwa na jambo hilo lazima atapewa placement mahali pengine nafasi itakapopatikana kulingana na sifa zake, kutoka kwenye data base!! Ni suala la muda tu!!
 
Kwa private sawa lakini government hakuna kitu kama hicho kuwa resources zitaisha hapana aseeh au kusema kuwa wafanyakazi wamezidi kuwa utendaji kazi utashuka hapa hizi ni governmental institute mzee hapo amfate mkurugenzi mkuu atapokelewa tu mshahara hautoki kwenye mfuko wa mtu huu
 
Ni kweli mishahara inatoka hazina lakini inakuja kulingana na bajeti iliyoidhinishwa!! Ukiongeza mfanyakazi mmoja bajeti ya kulipa mshashara wa huyo wa ziada haipo!! Hapa wenye kosa ni PSRS!! Kwa kuwa ni kosa lao watajitahidi kumpa nafasi nyingine itakayopatikana inayolingana na sifa zake!
 
Mkuu na wewe ni miongoni mwa wale barua zao za tangu mweI wa nne maana kuna mtu tulifanya nae mwezi wa pili kakuta barua ya mwezi wa nne mpaka nikasema inaonekana mzee alikuwa mgumu sana kusain barua
Hahah itakuwa Katibu ana mambo mengi thats why, coz hili dude la utumishi sio poa, pata picha kudeal na watumishi wote wa umma, sio poa kabisa

Mimi mkeka wangu ni wa mwezi wa 7 tu, Kaimu akaona afanye yake napema kabla mhusika mwenye mambo mengi kurejea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…