Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Hatimaye Nimelamba Asali ndugu zangu nawashukuru team ya hapa ndani kwa namna tulivyopeana moyo na kufarijiana na mimi niwape moyo kuwa it is just a matter of time. Nimekaa mtaani tangu 2014 mpaka sasa.

Mapambano yaendelee
Duuh Hongera broo... ukawe mtumishi mwema....naona uzi unazidi kupunguza wana tu
 
Nitoe rai tu, Kuna aja ya kuanzisha uzi kwa wale walolamba asali ili kutoa mwongozo kwa wengine wanaoendelea kulamba asali.

Hii itasaidia pia
1.Kutoa mwongozo wa kuchukua barua mapema, na nimetaka niongelee hili, nililamba asali ila nikatulia mpaka zile siku saba za awali zikapita, nikijua baada ya hapo barua itatumwa kwa njia ya posta lakini haikuwa hivyo.

Ilibidi niwapigie utumishi, baada ya muda mrefu wakapokea simu, wakasema bado hawajatuma barua niifuate, huku wakitoa sababu ya kuwa wasaka tonge hatuna anuani maalum, tunaweza kutuma kwa address ya Lindi, kumbe kwa wakati huo upo kigoma, kwahiyo kwa sasa kuna ugumu kidogo kwa utumishi kutuma barua ya placement kwenye box lako. "The earlier the better"

Hivyo nakushauri chukua barua ya mapema na ukaripoti kituo cha kazi.

2.Baada ya kuripoti kituo cha kazi uende na vitu gani?
Tofauti na vitu vilivyo ainishwa kwenye barua ya placement ni vizuri ukawa na balance kidogo, passport size, pitia hata standing order ili kujua stahiki zako kama first appointment employee, hii itakusaidia hata wakati wa kuomba posho za aina mbalimbali, kulingana na status na mshahara wako so ni vizuri ukajua hilo.

Pia ni vizuri ukawa na Bank Account kati ya CRDB au NMB, nilikuwa na tofauti ya hizo, ilibidi nifungue kati ya hizo mbili ndiyo zinatumiwa na Gvt kwa malipo ya mshahara.

3.Kwa upande wa halmashauri, kuna kurudi nyumbani wiki mbili baada ya kuripoti, hapa wewe ni mwajiriwa kabisa, sema kuna kasumba ya kuwa hawana hela ya kujikimu ya kukupatia hivyo unajaza fomu ya ruhusa ya lazima ile kwa wiki mbili then urudi kituoni kwa ajili ya kupiga kazi.

Sasa hapa mwenyewe nasubiria wiki ijayo nirudi kituoni kwa ajili ya kuanza kazi, lakini niliambiwa kabla ya kurudi nyumbani nikaongee na Mkuu wangu wa idara kupata ABCD.
"Karibu sana sema umekuja katikati ya mwezi kama ungewahi na taarifa zako kwa tarehe tano zikawa zimefika tamisemi, ungeweza pokea hela ya mshahara ya mwezi wa tisa na ukaanza kazi, hela ya kujikimu huwa inachelewa kutoka, yaweza chukua hata mwaka uipate.

Wewe rudi nyumbani, ikiwa utaingiziwa mshahara wa mwezi wa tisa wewe njoo kazini, ila kwa uzoefu na taarifa zako zimechelewa sina uhakika kama hela itaingia, ila kwa mwezi wa kumi uhakika na uje.

Wakuu nilitaka share nanyi kwa hayo, na wengine mwongezee, pia kama una risiti ya basi usiitupe, wakati wa kuandika barua ya kuomba posha mbalimbali, ambatanisha na hiyo, kuna jamaa yangu kaniambia alilipwa.

Hongereni kwa wanaolamaba asali pia Samahani kwa watafutaji, ila mtatoboa tu, nami nimesota sana na ujobless.
 
Thanks man
 
Shukrani mkuu kwa muongozo huu mzuri, hii standing order tunaweza kuipata wapi?

Sent from my CPH1937 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…