Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

..........Usimdanganye mwenzio.
 
Mfwende umemsikiliza yule mkuu wa kitengo cha IT ,utumishi kwenye clouds 360 alichoongea ? ,au kuna mwanajukwaa yoyote aliyemsikiliza yule jamaa ?
Mimi nimemsikiliza ametoa ufafanuzi mzuri sana kuhusu Usawa kwenye mchakato wote wa ajira, kanzi data, Integration ya necta, TCU & Nacte, Automation ya mfumo, involvement ya wataalamu tofauti kwenye oral na written, n.k in short ameeleza vitu jobless wangependa kusikia
 
Naomba nianzie hapo hoja ya mwisho.

Baada ya majina kutangazwa kwa Tovuti, na mitandao ya kijamii pia wahusika hupigiwa simu kujulishwa na kama mtu yupo mbali na hawezi kufika Ofisi za Sekretarieti huwa tunatuma barua za kuitwa kazini kwa anuani za posta walizojaza kwenye portal

Dhima ya Sekretarieti ya Ajira ni Kuendesha Mchakato wa Ajira kwa Haki na Usawa. Kila Mtanzania mwenye sifa za Kuajiriwa ana fursa ya kuajiriwa.

Nafasi moja huwa inawaniwa na wastani wa wasailiwa watatu.

Tunapotangaza Nafasi ya Ajira, kila mwenye qualifications znazohusika akiomba huwa anaitwa kwenye usaili wa awali wa Mchujo ili naye awe ametendewa Haki na Mchakato huu unaendeshwa kwa Haki na Usawa.

Ukifaulu kwenye Mchujo ndo hatua ya Oral hufuata.

Kila atakayefaulu kwenye Oral Interview kwa kupata alama kuanzia 50 kwenda Juu anakuwa na sifa za Kuajiriwa.

Nafasi zinaweza tangazwa 40 na katika hao wasailiwa waliofaulu 40 hujazwa kwenye hizo nafasi lakini wanaobaki huwa wanawekwa kwenye Database, kuna Vibali vya Ajira vya taasisi mbalimbali huwa vinatoka aidha baadae au baada ya usaili wa awali kufanyika hivyo badala ya kutangaza usaili mwingine basi wale waliopo kwa Database huwa wanachukuliwa na kupelekwa kwa hizo taasisi kujaza nafasi hizo.

Kwa sasahivi Database haijawekwa open kwa kila muombaji, lengo la kwanza la kutofanya hivyo ni kutowafanya waombaji kazi kubweteka kutoomba nafasi zingine za kazi zinapotangazwa wakichukulia kuwepo kwao kwenye Database kunatosha na hawana haja ya kuomba tena ajira. Database inadumu na majina kwa muda wa mwaka mmoja tu.

Maswali huwa hayatungwi na Sekretarieti ya Ajira, bali yanaletwa na Taasisi iliyopata kibali cha kuajiri na kukabidhi hilo Jukumu kwa Sekretarieti ya Ajira.

Kama kazi ni ya Kitaaluma bas maswali yanatungwa na wanataaluma husika japo sio yote huwa ni yale ya kuclaimisha darasani mengine yanapima uelewa wako. Na hata usaishaji mitihani huwa haisahishwi na staff bali wataalam mbalimbali kutoka vyuoni, au kwenye kada husika ambao nao hawakufahamu kwakuwa hua hatuandikishi majina kwenye karatasi za mitihani so ni kama Nekta.

Marks za Mitihani yote mnayofanya huwa zinawekwa kwenye mfumo na selection inafanywa kwa mfumo kwa kucommand mfano, watu 30 kutokana na high performance zao kushuka chini wakwanza had wa 30 kisha wanapelekwa kwa vituo vya kazi
 

Hiyo jumla umetupiga kamba
 
Sidhani kama kutakuwa na maswali mengine baada ya hii post,.japo hapo kwny uwazi wa database bado hapajakaa sawa.
 
Na upande wa status mbona hajagusa kabisa...
Not selected for Oral
Selected for Oral
Baada ya kutoka kukandwa oral
 
Hajaelezea kwa nini taasisi zinakinzana na psrs?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…