Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Mwezi wa nane waongezee majina maana kwa hii mikeka miwili itakuwa na watu zaidi ya mia 6 kiukweli masuala ya wazi itakuwa busy watatupumzika hadi wa 11 au wa 10 mwishoni huo mkeka wauongezee nyama

Kweli kabisa. Waweke majina yote ya mwezi wa nane hata mpaka wa tisa kabisa. Ili watu wapumzike pia hofu zipungue
 
[emoji23][emoji23][emoji23]yawezekana. Ila aongezee nyama hio kesho atushangaze
Duuuu naona kaweka mwingne tangazo la placement Linasoma tarehe 14 ila pdf inasoma tarehe 13 alafu ndan Majina yamepunguzwa kbsa..

Ya mwanzo ilkuwa na page 11 saiv Ina page 5 na baadh ya taasis hazipo na Majina

Nadhan alkosea...hizo ni human errors changamoto Kwa wale walkuwa Tyr washaupata mkeka na jina lake limo[emoji1]

Akichek saiv jina halipo duuuu u jobless ni shda sana
 

Kazi mnoo. Afu majina alioyapunguza, atayapost tena pdf lingine. Jumatatu sijui jumanne. Wale sio changamoto, maana ni uhakika nafasi yao ipo.

Sisi ambao hatujui siku wala saa ndio tunapata tabu. Maana hapo majina mengine hadi yaliyopunguzwa waitwe tena.

Wakipost majina mengi kwani ni kinyume cha sheria?! Au wanapenda kutupa psychological torture?!
 
Ule mkeka admin alioupost wenye majina zaidi ya 200+ wenye taasisi kama OCEAN ROAD,TAEC ,Wizara ya kulimo na Halmashauri nyingi.

Kiukweli Admin IT inabidi haupost tu Hana budi.

Maana atasababisha psychology torture kubwa kwa Jamii.

Maana tunao tayari na majina tumeyazumu.

Kwanini AFUTWE.

au nimshitaki kwa boss wake
 
mwenye case hii aenjoy coz kaona jina lake kwa lugha nyingine kishapata matokeo yake tyr. Akae kwa kutulia😄
 
Wadau naombeni ushauri tangu nipate placement kila saa akili inawaza SUBARU XT 2009 najaribu kufuta mawazo hayatoki nimejaribu kunywa beer nisahau ila ndio inazidi kunijia karibu zaidi.View attachment 2772942
Hahah mzee kaza buti tu, ujichange maana mimi na wewe hatupishani sana ila mimi fikra zangu ni kwa yule ndugu yake na huyo wa kuitwa Subaru Forester, ebhana kila nikiingia online nakutana nae😂

Siku si nyingi ntaanza kumuota sasa🤣

Ila all in all, tupambanie ndoto zetu, tusisasahau kuchapa kazi, kuepuka rushwa, ufisadi na upigaji

kusaidia wenye vipengele maofisini tulimo(kuna raia wana changamoto aisee tuwasaidie kwa nafasi zetu wanapokuja maofisini kwetu kufuatilia masuala yao) ,

na pia tuepuke mikopo umiza maana placement nazo hulevya, si unajua mwisho wa mwezi uhakika kwa hiyo unajilipua tu na mikopo isiyo na tija hivyo tujitahidi kujichanga na kuweka akiba.

#kaziiendelee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…