Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Mtusaidie mawazo na sisi fresher jamani, hivi inakuwaje mtu anafanya written interview, vilevile inakuwaje mtu anafanya oral interview?
Kikawaida au mara nyingi baada ya kukamilisha maombi kupitia ajira portal ya utumishi na kuwa na vigezo vile wanavyovitaka na kutuma maombi utasubiria kwa mda hadi uitwe katika usaili.

Mara nyingi hadi kuitwa inachukua muda wa mwezi mmoja hadi miezi mitatu.

Kutakuwa na saili za aina mbili.

Ya kwanza ni ya kuandika(written interview) na ya pili ni usaili wa mahojiano(oral interview).

Kufanya usaili wa kuandika huu hauna complications ni just baada ya kutolewa majina ya walioitwa katika usaili kwa kukidhi vile vigezo wanavyovitaka, na unatakiwa katika usaili uende na vielelezo vyote ili uruhusiwe kufanya usaili wa kuandika (written interview).

Baada ya kumaliza usaili wa mwanzo utasubiria kama siku 1-3 , watatoa matokeo ya written interview, ukifanikiwa kufaulu ndio utaweza kuingia katika hatua ya mwisho ambayo ndio usaili wa mahojiano( oral interview).

Hapo kitakachobakia ni kusubiria mkeka kwa walioitwa kazini unaweza kuwahi au kuchelewa.

N.B: Kuna kitu kinaitwa database au kanzidata hii ni kwa wale waliofaulu oral interview ila hawakufanikiwa kupata kwa mda huo kutokana na ufinyu wa nafasi za kazi ila watapangiwa sehemu nyengine ndani ya mwaka mmoja ikiwa nafasi zitapatikana.


Pia kuna usaili wa vitendo baada ya written interview kwa wale kada zao zinazohitaji practical.

So pia sometimes kuna saili za aina tatu, yaani written, practical and oral interviews.

Ili uende katika hatua nyengine ya usaili lazima ufaulu kwa kila hatua.

Nadhani nimekujibu vyema ndugu yangu.
 
Daaah kaka asante sana umenijibu vyema kabsa, nmepata mwanga tayari
 
Wakuu naona wengi wenu humu mnapotoshana sana kuhusu kupata Ajira na uhusiano na Mungu

Ajira sio Mambo ya kiroho, ni mambo ya Matendo, naona mnaanza kupeana Hope ambazo haziwezi kuwasaidia katika hili

Kuna zaidi ya 70% ya wanaopata Ajira utumishi hawajawai kwenda kwenye mkesha,hawajawai Kufunga mfungo mtukukufu,na wala hawajawai kuwa swala 5 na wala hawajui mafuta ya mwamposa yanafananaje

Mtu atapata kazi alafu atakwambia ni Mungu tu kusema ukweli me nilifanya vibaya ila niliamua kumrudia Mungu,niliamua kumlilia Mungu,niliamua kusema na Mungu

Come on brothers and sisters, hii mitihani ya Utumishi sio rahisi kama tunavofikiria na wala sio migumu kama tunavyoichukulia, ukitaka kujua mitihani ni migumu angalia marks za Written, kuna watu wanapata hadi 1 au 9 na alijiandaa huyo usidhani yeye kazi alikuwa haitaki

Kupata Ajira ni swala la Performance, Ukipata kazi jipige kifuani kwa sababu ulipafomu kuliko wengine, hizi mark's za oral ni Siri ila ukweli ni kwamba ukitaka kujua reality we angalia mark's za kwenye Written basi utajua kuwa ata kwenye Oral kuna watu wanafeli pia tena sana tu

Unaweza kujihisi wewe hukufanya vizuri ila uhalisia ni kwamba kuna aliefanya vibaya zaidi kuliko wewe, hizo marks zako 40 ndio zimekupa kazi na kumnyima aliepata 20 kushuka chini

Mara ya pili hii nasisitiza wekeza katika kufika Oral, kwenye Written tumia mbinu zozote ambazo haziwezi kukuharibia ili ufike Oral, weka kijiji,igilizia nk ili Tu ufike oral, kwenye oral kuna watu wengi sana hujitoa wenyewe kwenye mashindano kwa sababu mbali mbali

Ukikaa na panelists wanaosimamia oral wakakupa tathmini ya watahiniwa unaweza kucheka na kushangaa inakuaje mtu ana bachelor ya kitu Fulani na hawezi kujielezea, kuna muda hadi wao wanafanya adjustment tu ili waweze kupata watu wanaowataka

Kuna kundi kubwa la watu wakiwa kwenye oral ata sauti waga hazitoki ila hawezi kuja kukwambia,kuna kundi kubwa la watu wakiwa kwenye oral wanaishia tu kusema Dahh/Mungu wangu hakuna point wanakumbuka ila hatokwambia, kuna kundi kubwa la watu wakiwa kwenye oral waga wanakumbuka point 1 Tu kila swali ila hatokwambia, kuna kundi kubwa la watu kwenye oral waga wanapanick na kuanza kulia Tu hadi dakika zake zinaisha ila hawatokwambia

Ndomana ukichunguza kwenye Oral kuna ambao waga wanakaa sana na kuna ambao waga wanakaa kidogo Tu unashangaa katoka, kiufupi ni kwamba wanafunzi wa kitanzania kwenye Oral tuko shallow sana, zaidi ya sana kwahiyo jitajihidi sana kujitofautisha na wengine ili wewe uwe katika kundi la wenye unafuu

Kwahiyo kwenye kundi la watu wa namna hiyo ukitokea wewe ambae utaweza angalau kujibu points 2 kwenye kila swali basi unapata kazi yako kiroho Safi bila shida yoyote maana wewe ulikuwa ni mwenye nafuu kuliko wengine, utumishi wakiamua kufata taratibu zote basi watarudia sana kutangaza kazi

Mungu hawezi kubadili 25% ikawa 60% Mungu hawezi kubadili point ya Uongo ikawa ya Kweli, Mungu hawezi kubadili kingereza chako cha hovyo kikawa kizuri katika chumba cha mtihani, mtataka kumpa lawama za bure tu Mungu wenu

Kwakuwa watu watakaopanick kwenye oral lazima wawepo tu hiyo ni pie, basi wewe tumia udhaifu huo kujinoa vile utaona inafaa ili usije kuwa katika kundi la wanaopanick hovyo, jua ni namna gani utaweza kupunguza pressure,jua ni namna gani utaweza kuwa relaxed during interview, ikiwezekana jifunze body posture and body language

Nakupeni Siri tu ambayo itawasaidieni, Asilimia 60% ya wanaopata kazi utumishi sio kwa sababu walifikisha cut off points, lahasha kwa sababu wao walikuwa na unafuu sana kuliko wengine, tuliopata kazi kupitia utumishi tunalijua hili, kuna muda hadi unaona Huruma kwani aliekusaidia kwenye written hadi ukaingia kwenye oral yeye anakosa kazi naww unapata na unajua yeye ni Bora mara 100 zaidi yako
 
umeongea point
 
Naishi nayo hii🀨
 
Wakuu nimeshafanya oral interview,
Kwenye web status bado iko SELECTED FOR Oral interview then kwenye app Status inasoma NOT SELECTED for oral interview. Hii inamaanisha nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…