Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Mikeka mingi ya mwaka huu itaanza kuchukua watu wa Jan 2023 nakuendelea
Hawa Jamaa hawaeleweki inshort ila wanazidi kujitangaza , huku kwa wasaka ajira ni taabu tupu....
Na Usikute wanatumia mgongo wa kuhamisha wafanyakazi wa mashirika waliofuta kupitisha ndugu zao hizi pdf zinazotoka.....
 
Usilinganishe Wazungu na watu wengine. Hao ni level nyingine kabisa kwenye ustarabu na kujali ubinadamu.
 
Utumishi wako radhi wafanye interview kadri ya wawezavyo ila majina ya kazi wanaita kiduchu.

Na wanajaza rundo la watu kwenye database.

Umeshakuwa ugonjwa wao sasa.
 
Asante sana Mkuu
Ila hiyo Baba Jane bye bye jamani[emoji3061][emoji3061]
Asa mtu oral tokea mwezi wa kumi huko Hadi leo listatus linasoma Selected for oral interview both app&web adi mtu anashindwa kuelewa yaani miezi Kama 5 imekata.
[emoji16][emoji16][emoji16] miezi 5 unaona ni miezi mingi sana ehhh

Wengine hapa tulifanya Oral mwezi wa Kwanza 2023 placement ikaja kutoka mwezi wa 11

Na kuna ambao tulifanya nao hadi leo hii bado wanasubiri
 
[emoji16][emoji16][emoji16] miezi 5 unaona ni miezi mingi sana ehhh

Wengine hapa tulifanya Oral mwezi wa Kwanza 2023 placement ikaja kutoka mwezi wa 11

Na kuna ambao tulifanya nao hadi leo hii bado wanasubiri
Yaaani ni masikitiko mwaka mzima mtu anaingia web ya utumishi
 
Yaaani ni masikitiko mwaka mzima mtu anaingia web ya utumishi
We ukifanya interview yao achana nao endelea na mambo mengine ambayo ulikuwa unafanya au endelea kutafuta issue zingine za kujitafutia Ridhki

Usiwe na matarajio makubwa sana kwa sababu hiyo kazi hujaomba Peke yako, na sio wewe tu ndio mwenye uhitaji bali ni ule umati wote uliokusanyika siku ya tukio

Maana halisi ya interview ni MCHUJO, kwahiyo ukilijua hilo huwezi kujipa pressure kwa sababu unajua ulichofanya ni pata potea na hamuwezi kupata wote ata kama watatoa majibu ndani ya week 1

Kwahiyo kuchelewa kwao kusikufanye uache kufanya mambo mengine, usisubiri hadi mwaka upite ndio ushtuke kutafuta kitu kingine cha kufanya, muda haujawahi kuwa Rafiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…