Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Ukisoma matangazo ya ajira unaweza kutukana bure...
Wizara ya elimu ilitoa nafas 58 toka January...leo April hawajaita watu interview
 
Habari za Saizi jamani ?
Naombeni kuuliza ndugu zangu mm hapa nimeitwa usahili wa mchujo utafanyika hapo kesho kutwa Sasa Sina kitambulisho Cha NIDA kwa sasaiv na ninacho Cha kura lkn hakifanani mwaka wa Kuzaliwa na cheti Cha Kuzaliwa naona kama nikionyesha pale nje kabla ya kuingia kwenye usahili wakati wa kuhakiki wa vyeti kinaweza kuniletea changamoto japo Sina uhakika kwa mwenye kujua atanisahihisha juu ya hili .Sasa naomba kuuliza ninaweza kuomba barua kutoka kuandika barua kutoka ofisi ya Kijiji niliko Sasa ambako nimekuja tu kwa mda mfupi sio kama ni nyumbani kbs kbs ? Naombeni msaada wa kujibiwa ndugu zangu
 
Kikubwa majina yafanane, majina yaliyoko kwenye cheti na kitambulisho cha NIDA yafanane
 
hakuna mtu anayekagua tarehe ya kuzaliwa pale usisumbuke bure
 
Kuelekea Kesho maazimisho ya Muungano ...PSRS mnaamua kutulaza gizani kwel, kwa machungu vijana wenu bila mkeka mzito wa taasisi tupate faraja😥😥😥
 
Kuwa na NIDA sio lazima. Ila kinachohtajika n utambulisho...
Cha kufanya Nenda Serikali ya Mtaa wakuandikie barua ya Utambulisho iwe na majina ya vyeti vyako na katika barua wanaweza andika huyu mtu ana NIDA namna fulani hyo namba ya nida kama unayo waiweke tayari ushamaliza kazi. Barua hyo itasimama kama mbadala wa NIDA nk. Ila hakikisha majina anayoandika yasiwe na tofauti na majina ya vyeti.
Pia sikuwa na NIDA ila mara mbili naingia usaili mpaka oral bila kitambulisho na wanapokea barua.

Kila heri
 
Kuna mtu niliwahi kukutana nae tumeenda kuchukua barua ya placement walimkatalia kumpa barua licha ya kuwa na barua ya serikali ya mtaa pamoja namba NIDA walimwambia aende akalete kiapo kinachoonesha hiyo namba NIDA ipo sahihi jina lake
 
mmhh wako makini kwenye barua inaonekana kuna mtu ashawahi kumlambia mwenzie asali 🤣 🤣
 
Kuna mtu niliwahi kukutana nae tumeenda kuchukua barua ya placement walimkatalia kumpa barua licha ya kuwa na barua ya serikali ya mtaa pamoja namba NIDA walimwambia aende akalete kiapo kinachoonesha hiyo namba NIDA ipo sahihi jina lake
Duh hapo sasa ni kuwa na vyote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…