Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Ongera sana sana ndugu.

Nasikia sauti kwa mbali inaniambia na mimi pka mwezi wa 2 nitakua nishalamba hasari.
Inshallah imani inaponya, kati ya kitu kilichotaka kunipoteza, nilipomaliza chuo nikakutana na kale ka skendo au kausemi ka wahitimu wengi kwamba ajira hamna, sijui mpaka uwe na mtu huko ndo unaweza kupata, eeh bwana eeeh nami nilijaa kwenye mfumo nikarudi kwetu bhana🤔Lakini maisha yaliponiponda na zile kero za nyumbani😌 Mala ooh naomba unisaidie kuosha vyombo🙄 n.k n.k, baada ya hapo ilibidi nijiulize swali moja " Hivi nimesikia story tu kwamba siwezi ajiliwa mpaka niwe na mtu kule Je, nimejaribu? Uhakika ninao wa hayo maneno? Nimeanzaje kuamini sijaanza fanya utafiti mwenyewe?" Baada ya hayo maswali machache kati ya mengi niliyojiuliza nikageukia Jamii forum ( jamii forum huwa nakimbilia sana kupata majibu ya baadhi ya maswali kwa sababu humu uwezo wa kupata ushauri bila nyodo ni kugusa na huku unakutana na baadhi ya watu wanaopitia unayopotia wewe Kwahiyo mtu akikushauri anakua na Experience) eeh bwana eeh sinikakutana na huu Uzi, nikaanza kufuatilia mdo mdo na hapo kipindi hicho nilikua nahangaika na akaunti yangu Ajira portal maana kila nilipokua najaza taarifa asilimia zilikua hazipandi bali kuishia 70% kumbe nilikua nasahau kuweka cheti cha form four 😁 baada ya kukumbuka hilo na kukiweka mambo yakatiki buana asilimia zikasoma 92🤗 nami nikasema "Unyama "😎 sasa huu uzi ukazidi kunijaza kifua nikajikuta kumbe nilichelewa 🥴 ilikua mwezi wa kumi na moja kama sio wa kumi na mbili 2023 zikatoka nafasi kwenye kada yetu na zilikua 20 MDAs and LGAs, ooh nikasema hawa naanza nao nikaaply ikakubali baada ya hapo mwezi wa pili tarehe 20 nikafanya usaili wangu wa kwanza serikalini😁( kwenda kuomba Hela ya usafiri kwenda dodoma kwa mzee alinambia " Sawa nakupa lakini sidhani kama utatoboa" nae alikua na kale ka Imani ka kijinga kanakopoteza wengi😂 kimoyo moyo nikasema nitakuprove siku moja😎)eeh bwana eeh kale ka presha kakaniharibia buana mpka natoka kwenye chumba cha usaili najisemea rohoni huku nikikumbuka usemi wa huu uzi kwamba "Nimekandwaaa"😃, tena nikasema kwamba naanza kuisahau Dodoma sitokuja kukanyaga tena huku🙄🤔baada ya kufika nikajishauri huku uzi huu ukizidi kunipa moyo kwa uchangiaji wa wadau hasa shuhuda za watu humu😃 Karoho kakajaa tenaaaa mala TANAPA hawa hapa wanataka watu 15, nikajaa kwenye mfumo, mchakato ukakamilika wa saili hapo hapo nikiwa nimemwambia mungu wangu kwamba safari ya TANAPA asinitupe bali awe nami bega kwa bega🙏🙏na kweeli mwenyezi Mungu amekua nami bega kwa benga mpaka nimepata nilichomuomba na kuambatana nae🤗
 
Kuna jambo la kujigunza hakika
 
Mkuu umeingia juzi tu kwenye mfumo (ajiara portal) tayari ushatoka hongera tena kwa mara ya pili
 
Wakuu naombeni ushauri, mimi nina kazi private sector (start up). Ni kazi ambayo haina mkataba wala pension (ni miaka miwili sasa), tuliongea tu kwa mdomo. Nalipwa kama 600k hivi, sasa naona startup yenyewe haitusui, na nina mke na mtoto mmoja. Nahisi kama napoteza muda. Nina diploma ya computer science, na kazi karibia 99% za IT PSRS zinahitaji degree.

Nime apply sehemu tatu LGA (mshahara 580,000 position (60)),
NIT (mshahara 860 hivi position moja), chuo cha bahari (mshahara 1,300,000 hivi kama sijakosea | position moja).

Sasa maswali yangu ni:-

  • Nibaki startup, hoping for the best bila pension na umri unaenda kwa hope ya kutusua huko mbele?
  • Niombe mkopo nisome degree. (Kama nitapata)
  • Nisifanye interview ya LGA kwasababu mshahara ni uleule wa mateso?.
  • Nifanye LGA at least nitakua na pension, bima ya afya na nitajiendeleza huko mbele?.
  • Nifanye tu interview za taasisi (NIT, DMI)?.
  • Nisitegemee sana position hizo moja moja?.
 
Pambana uwezavyo uingie government
 
Brother, tupe tips za oral interview
 
Tupe mrejesho wa Mshua baada ya kumpa hii taarifa ya kuangukia Mbugani za Wanyama, amesemaje tena[emoji23]
 
Pambana uwezavyo uingie government
Naongezea hapo, Kwenda kusoma degree ni kupoteza muda, Unauliza mfilisiti unamaana gani? Kuingia serikalini ni rahisi sana ukiwa na diploma kuliko degree, degree kuna ushindani mkubwa sana, hapo tu wewe umesema kuna nafasi 60 LGA, ni nadra sana kukuta hizo nafasi kwa degree! Asomaye na Afahamu mangoEmbe
 
Baki hapo Startup.

Omba nafasi PSRS kila zinapotangazwa.

Hudhuria saili zote utakazoitwa

Ukipata nafasi hata ya hela unayoona ni ndogo huko Gavo, nenda kapige kazi.

Gavo na huo huo mshahara unaosema ni mdogo, utapata Bima yako na familia yako. Kwenye matibabu hutotoboka hela, labda case iwe kubwa sanaa na Bima ishindwe kuhandle.

Usiende kusoma kisa unafukuzia kuja kutafuta kazi, yaani usiende kusoma huku hauna kazi. Kusoma kwa kujiendeleza ni vizuri ukiwa na kazi/unatokea kazini kwa ruhusa ya mwajiri huku maslahi yako yakiendelea kupatikana.

Kila la kheri kwenye maamuzi yako
 
Yeah kweli mkuu. Asante sana.
 
Sawa chief nimeupokea ushauri wako asante sana.
 
Umemaliza kilakitu ndugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…