Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Oyaa kaangalie pdf mkuu huenda upo ufunge mwaka kibingwa
 
Huu uzi ni sehemu salama sana kukupa a, b, c kuhusu interview za psrps

Mimi ni mgonga ulimbo ambae sijakata tamaa kwa mara ya kwanza nilishiriki mchakato wa interview za psprs kwa kada yangu ya afya mwezi december nikaliwa kichwa kwenye written tu😁nilihisi kukata tamaa sema mtu wa maana sana humu Mwifwa katika baadhi ya post zake alisisitiza kutokata tamaa na tusiache kutuma maombi.

Nikatuma maombi kwenye post moja ya chuo cha serikali mjini dsm, Mungu si Athumani nikaitwa kwenye usahili zingatia wanataka mtu mmoja tukaitwa 317

Nikakumbuka tena bro Mwifwa husema hata kama nafasi moja kashiriki interview sikuwa nimesoma chochote nikashiriki na tukafika watu 127 tu kwenye usahili wa written

Nikafanya ila sikuwa na matumaini ya kuitwa oral bahati nzuri tukachaguliwa watu 12 kwa ajili ya oral ambayo naifanya soon.

I wish kupata a, b, c, d kuhusu oral interview za psprs maana hii ndio inaenda kuwa ya kwanza kwangu.

Natanguliza shukrani
 
Pita apo Mkuu unaweza pata kitu
 

Pitia uzi aliosuggest mdau hapo juu. Pia usisahau kufanya rehearsal. Anza kufanya practice ya namna utakavyokua unajibu especially kwa maswali ya mwanzo ya utambulisho na kutaja responsibilities. Ni kweli hujui maswali gani yatakuja ila ukijiandaa namna utakavyokua unaflow, inasaidia kuboost confidence na kuonekana unajua unachokisema.​
 
Asante sana mkuu
 
Hongera sana mkuu, kila la kheri kwenye hatua hiyo mbeleni.

Hints nyingi tushazitoa humu, ukiweza kurudi nyuma kwenye uzi kuanzia September 2022 kuja mbele utaona hayo madini ya hints
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…