HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Nimeliwa kichwa kwa nafasi ya TAA, ninasubiri majibu ya NEMC. Kisha nitasubiri kuitwa kwenye interview ya MDAs & LGAs. Ikiwa zote hizi nitashindwa kwenda oral interview basi ninadhani safari yangu ya kuomba ajira itakuwa imeishia hapo. Mwaka wa 9 huu toka nivae joho bado patupu. Ni vema nikubali tu kwamba ninapaswa weka juhudi na kuendelea kupambana zaidi na hiki ninachokifanya sasa, sio lazima niingie kwenye ajira.
 
Uwwwi basi mie najiona nimesotaa kumbe watu mna miaka 9 wallah dah,tusikate tamaa kaka yangu japo inaumiza sana lakin tupambane ipo siku yetuu naamini hiloo
 
Hii ishu ya kusaidia watu kwenye Application sometime ina disappoint.

Bora huyo alihudhuria mkando.

Mimi kuna watu nimewasaidia kufanya application na kumanage kila kitu kuwahusu kuhusu Application, ila mwisho wa siku hawatokei kwenye mkando.

Watu wa hivyo nishananwa mikono, bora niendelee kupiga soga hapa na wapambanaji wengine
 
Lawama zote zinaangukia kwako kuwa kuna kitu ulikosea πŸ˜‚
 
Mkuu tokea mtu afanye oral mpk kuitwa kazini huwa inachukua muda gani kwa uzoefu?
Hata mwaka inaweza kufika kikubwa ni kuchungulia chungulia kila mkeka utumishi wanaotoa. Kama ulifika oral chance ya kupata au kukosa ni 50% unaweza usipangiwe ile kazi uliofanya interview lakini ukabaki data base siku nafasi nyingine ikipatikana wanakuchukua kuijaza so inachukua muda sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…