HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

hamu yote ya placement imeniisha kama umeme wenyewe ndo hivi si hatari hii..
😅😅😅
 
Uko na hali mbaya bro, kama ww ni graduate engineer wa electrical halafu pasi tu inakushinda , duh.
Anyway anza kukuza skills zako usijeaibika.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] we jamaa unachangamsha sana.
 
Leo katibu mkuu utumishi Bw. Juma S. Mkomi kawatolea uvivu wote wanaochelewesha kuajiri kwa sababu zisizoeleweka wakati kabla ya kuomba kibali wamekua wametoa bajeti na kuandaa kwenye P.E .

Hali hiyo imetokana na malalamiko ya muda mrefu kwa vijana walioajiriwa na kupata barua zao lakini kukubaliwa na kuanza kazi kuna kuwa na vikwazo vya kumsubirisha mtumishi mpya kwa muda wa kufikia mpaka miezi 6 ili tu mwaka wa fedha ubadilike.

Aidha, Ametoa rai kwa waajili wote wawapokee watumishi kwani waliandaa bajeti ya kuajiriwa na kisha kuomba kibali kwa katibu mkuu utumishi.

Sambamba na hilo, Amesema kuna hali ya wasailiwa kuomba kazi mara kwa mara kwa kutotambua iwapo wako kwenye kanzidata ama hapana hivyo kupelekea wasailiwa kutumia fedha nyingi katika mchakato mzima wa ajira wakati tayari unaweza kuta msailiwa huyo amefaulu na yuko tayari kwenye kanzidata.

Vilevile, Waajiriwa wameaswa iwapo wana vijana wao wanaojitolea na hivyo kupelekea kukataa waajiriwa walioletwa na sekretarieti ya ajira yaani psrs inabidi waombe kwa kufuata utaratibu wa kuwaombea vijana hao ajira na sio lazima wakubaliwe maombi yao kwani ni utashi wa katibu mkuu kuridhia maombi hayo ama kukataa.
Pamoja na hali hiyo waajiri wameshauriwa kutotumia mwanya wa vijana wanaojitolea kuchelewesha ama kuendelea na kukataa waajiriwa wapya waliopambana na kupata kazi kwani hali hiyo haikubaliki. "Utajiskiaje kijana wako anafanyiwa jambo hilo wakati amefaulu usaili na amepata barua ya kuajiriwa? Bw. Mkomi amesema.

Katika kumalizia kikao hicho na washauri wa waajiri amesema kigezo cha kusingizia uhakiki wa vyeti sio kweli kwani mifumo haifanyi kazi hivyo. Pia amesema wakipata taarifa za muajiriwa mpya kucheleweshwa kuajiriwa watadili na muajiri kwa kufuata sheria kanuni na taratibu.

Link ya video hiyo

View: https://youtu.be/110Tv8nImIA?si=azEQ6uZQEfh-hck2
 
Jobless umepigwa na shoti, hatari na nusu, hiyo ni dalili nzuri. Unalamba asali soon Engineer
 
Dah. Afadhali, maana miezi miwili inakata, kila ukimcheck anakuambia usiwe na haraka Afisa. Yaani unapewa cheo kikubwa wakati nipo mtaani naendelea kuchakaa. Dah!
Wamepewa maelekezo makali sana. Waache uhuni, yawezekana katibu mkuu anasoma huu uzi.
Anadai vijana wanakopa nauli kupigania mchakato mwishowe anapata kazi baada alipe madeni, mnamchelewesha kumuajiri kwamba mnasubiri mwaka mpya wa bajeti kanakwamba hawakuoanga bajeti kabla ya kuomba kibali.
 
Hii ngoma ni kweli wengine tuna miezi 7 ......
 
Inamaana hata sisi tuliofanya June 10, tutaitwa mapema
Hapo anazungumzia baada ya kupata 'placement' ukiripoti kazini kulikuwa na utaratibu wa kuwasubirisha ajira mpya kwa muda mrefu hadi zaidi ya miezi sita bila sababu za msingi.

Kwa sasa waajiri wanatakiwa wakishampokea mtumishi baada ya kuripoti kazini wafanye mchakato wa kuanza kazi haraka iwezekanavyo sio kuendelea kusubiri wa miezi kadhaa.
 
Jamani hivi kuitwa kazini kama ulifanya oral kupitia taasisi means na kaz utapat za taasisi pekee

Sikufanikiwa kwenda oral ajira za MDA & LGA za mwezi september 2024 kada afya

Nikaja kupita kwenda oral ajira ya taasisi ,ambapo walitak mtu mmoja na washampata

Sasa kila pdf nalolizoom naona wanaoitwa kazini ni wale waliofanya oral ya LGA & MDA ni kwamba sisi wa oral ya taasisi japo kada moja tupo sawa tu na wadau wa not selected majina yetu yanawekwa kapuni au inakuaje

Nimechok kupitia pdf kwa kweli
 
Kwahiyo kumbe sisi haituhusu🤕
 
Oral ulifanya tarehe ngapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…