Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Wakuu nimetoboa Alhamdulillaah, ambao hamjapata nawatia moyo, sitasahau huu uzi umenipa matumaini sana.
Hongera sana mkuu. Kila la kheri ukawe mtumishi mwema na bora, kazingatie maadili na miiko ya utumishi. Zile nyodo na majivuno siyatarajii kwa mpambanaji wa namna yako, hayo mambo waachie wanaovutwa kwa mserereko bila kujua msoto wa kupambana.

Usisahau kuja kutujulia hali humu tunaoendelea kupambana, kila mmoja ana siku yake ya kutoboa, hatuwezi kutoboa wote kwa siku moja. Tangulia tutakuja siku yetu ikifika!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…