Kwanini vijana wadogo sasa wanapata magonjwa yasiyoambukiza?

Joined
Jul 21, 2019
Posts
58
Reaction score
72
Habarini wanajamiiforums,

Hivi sasa kumekuwa na ongezeko la magonjwa yasiyokuwa ya kueneza (non-communicable diseases) kama vile kisukari, shinikizo la damu na kufeli kwa figo miongoni mwa vijana wadogo wenye umri wa kati ya miaka 20-35.

Je, unahisi wapi tunakwama na tufanyeje kujikwamua kwenye hili janga?

Karibuni.
 
Ata zamani watu walikua wanaumwa na kufa, zamani walikua wanakufa na hatujui kichowaua, maendeleo ya science na technology ndiyo sasa tunajua wanachoumwa. Ni hivyo tu
 
Hayo ni magonjwa ya mtindo wa maisha.Inategemeana na unachokula na kunywa. Watu wengi wanaamini kuwa wanakula vyakula bora kumbe wanakula hovyohovyo.Kwa hiyo ulaji usiofuata kanuni na mpangilio matokeo yake ndiyo hayo.

Vyakula vingi vinavyoandaliwa kwa kutumia mafuta ya wanyama na hata ulaji wa nyama wenyewe (nyama nyekundu) ni hatari sana kwa matumizi ya baadaye kwenye mwili. Lakini pia asilimia kubwa sasa hivi tunakula na kunywa sana sumu kupitia vyakula vya viwandani.
 
Maendeleo ya sayansi na technolojia yamechangiaje ongezeko hili?
 
Hayo ni magonjwa ya mtindo wa maisha.Inategemeana na unachokula na kunywa. Watu wengi wanaamini kuwa wanakula vyakula bora kumbe wanakula hovyohovyo.Kwa hiyo ulaji usiofuata kanuni na mpangilio matokeo yake ndiyo hayo.

Vyakula vingi vinavyoandaliwa kwa kutumia mafuta ya wanyama na hata ulaji wa nyama wenyewe (nyama nyekundu) ni hatari sana kwa matumizi ya baadaye kwenye mwili. Lakini pia asilimia kubwa sasa hivi tunakula na kunywa sana sumu kupitia vyakula vya viwandani.
Umenena mkuu
 
Back
Top Bottom