Kwanini viongozi na wanachama wa CCM hawashangilii ushindi mkubwa wanaoupata Serikali katika kesi ya Mbowe? Ukimya wao unamaanisha nini kwa Serikali?

Kwanini viongozi na wanachama wa CCM hawashangilii ushindi mkubwa wanaoupata Serikali katika kesi ya Mbowe? Ukimya wao unamaanisha nini kwa Serikali?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Yapo Mambo ukiyaangalia Kwa macho ya ROHONI unatambua Yana fumbo kubwa Sana. Mbowe ni mhalifu aliyekamatwa na serikali ya makini ya awamu ya sita,akafikishwa mahakamani, akasomewa mashtaka, akakana, serikali ikawasilisha ushahidi, ikapata upinzani mara mbili nakupelekea mahakama itoe hukumu ndogo dhidi ya mapingamizi yaliyowekwa, Mhe. Jaji akaonyesha mapingazi yote serikali kupitia Mawakili makini wameshinda....hakuna Kiongozi wa serikali ya awamu ya Tano aliyejitokeza adharani kushangilia utendaji mzuri WA Mawakili wa serikali.

Hakuna aliyeandika hata kwenye mtandao wa kijamii kuonyesha kuipongeza mahakama Kwa KAZI nzuri ya kutoa Haki, hakuna chombo kinachomilikiwa na chama au serikali kilichotoka adharani nakutafuta maoni ya Wana CCM na serikali yao kwenye ushindi huu.

Hii ni tofauti na kesi nyingine ambazo serikali ushinda, tumezea comments nyingi sana kutoka serikalini lakini this time wote wamekaa kimya hakuna anayetaka kujadili kabisa maamuzi. Najiuliza haya maamuzi anayotoa Jaji kwenye hii kesi kwanini ayapongezwi? Kwanini watu wamenuna hata waliopaswa kushangilia?

Mashahidi wakaendele kutoa ushahidi wao na leo ikatolewa maamuzi kwamba watuhumiwa wote Wana kesi ya kujibu. CHADEMA wakashangilia kwamba mapambano yanaendelea. Upande wa Jamhuri hakuna aliyeshangilia au hata kuthubutu kutabasamu. Walioshindwa wakaonekana wanafuraha KULIKO walioshindwa...what's wrong with you winners? You are discouraging our Prosecutors and Judges for your quietness.

Mnamfanya Jaji ajiulize labda ajaeleweka? Mbona anatoa hukumu mnanuna? Hata vyombo vya habari navyo vinaripoti Kwa uoga. Who is Mbowe? Ambaye anaitwa Gaidi lakini Wananchi awapendi ahukimiwe Kwa makosa yake?

Tuachane na Wana CCM kushindwa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya Tano, twende kwenye MAPOKEO ya maamuzi ya mahakama. Wananchi wanaposhangilia kumpongeza Mtuhumiwa wa Ugaidi unajiuliza nao ni magaidi? Shangwe hizi na nderemo zakumtia Moyo Gaid zinatoka kwa Wananchi Gani? Kama serikali inalinda raia na Mali zao kwanini wasikamatwe wanaoshangilia wahalifu na kuwatia Moyo? Hawa Wananchi kwanini wanapingana na viongozi wa wao.

Mwisho tujiulize, hao watanzania wanaomtuhumu Mbowe kuwa ni Gaidi wapo wapi? Mbona awashangilia ushindi mkubwa kiasi hiki? Mbona ushindi huu umewanyima wananchi amani? Hatuoni kama wenye furaha ni watu wachache sana Tena ambao ukiwaliza furaha Yao inatoka wapi awawezi kukuambia?

Naamini yupo Kiongozi ndani ya top Three za awamu ya sita wangekabidhiwa nchi Cha kwanza wangefuta kesi hii baada ya kuona wananchi wameshindwa kabisa kuyaelewa maamuzi ya Jaji. Kibayazaidi kinachowafanya wananchi washindwe kumwelewa Jaji ni pale anaposoma au kutoa summary ya maamuzi bila kutaja sheria au kanuni, bila kueleza ushahidi upi ulikuwa na nguvu na mazingira au vielelezo Gani vilijitosheeleza. Inshort Jaji alichofanya kikawachanganya wananchi ni pale aliposoma

1. Mashataka,
2. Akasoma watuhumiwa
3. Akasoma majina ya Mawakili,
4. Akasoma majina ya mashahidi,
6. Akasoma vielelezo
7. Akasema yeye binafsi not sheria
8. Ameona watuhumiwa Wana kesi ya kujibu.

Hapa ndipo utata ulipoanzia, kwamba Jaji Hana kifungu Cha sheria, Hana analysis ya kufikia maamuzi na Hana sababu ya kwanini Wana kesi ya kujibu. Hii haijawahi kutokea mahakama Kuu yoyote Duniani may be Tanzania.

Lakini Juzi nilijiuliza siku mbili zinatosha kusoma kurasa 1500? Leo zimeombwa siku sababu za kuandika maamuzi means kutokuonekana analysis yoyote ni matokeo ya kutokusoma. Lakini kilichosomwa leo kimeshindwa kueleweka masikioni mwa wengi Kwa sababu Dunia yenye watu wenye akili ilishaacha kuambiwa. May be ndio maana CCM wanakuwa mabubu kwenye hii kesi maana Awana point yakusimamia labda warushe ngumi
 
Hapa ndipo utata ulipoanzia, kwamba Jaji Hana kifungu Cha sheria, Hana analysis ya kufikia maamuzi na Hana sababu ya kwanini Wana kesi ya kujibu. Hii haijawahi kutokea mahakama Kuu yoyote Duniani may be Tanzania.
 
Lakini Juzi nilijiuliza siku mbili zinatosha kusoma kurasa 1500? Leo zimeombwa siku sababu za kuandika maamuzi means kutokuonekana analysis yoyote ni matokeo ya kutokusoma.

Lakini kilichosomwa leo kimeshindwa kueleweka masikioni mwa wengi Kwa sababu Dunia yenye watu wenye akili ilishaacha kuambiwa. May be ndio maana CCM wanakuwa mabubu kwenye hii kesi maana Awana point yakusimamia labda warushe ngumi
 
Kwanini CCM hawashangilii?
1. Pamoja na ukatili uliokithiri , CCM ni wanadamu wanaojifunza .

Mh wa shule ya uongozi alikuwa maarufu sana na hasogeleki.
Ilichukua miezi kadhaa siku hizi akitembea anaangalia nani anakuja nyuma.

Mh. Nnauye, alikuwa Waziri asubuhi, jioni anakumbana na kitu chenye madini ya Zambia.

Mh. Christian Bashite, alikuwa katika hadhi ya naibu fulani, siku hizi anajificha kama digidigi.

2. CCM wanaona ukiukwaji na kuingiliwa kwa mfumo wa kutoa haki.
Kama wanadamu wanajiuliza ikitokea kwao au ndugu zao hali itakuwaje?
Mfumo ule ule utakuwepo

3. CCM wanaona kesi imezidi kuwapa nguvu Wapinzani. Wakiangalia hamasa ilivyo, ni wazi badala ya kubomoa huenda inajenga. Nao wanajua upinzani imara ni madhara kwa nani

4. CCM wanaona kesi kabebeshwa Mh Mwenyekiti wao.
Hilo linaharibu taswira ya chama na wanajua ugumu wa ushindi bila goli la mkono la Nape.
Wanajua mwendazake alivyotumia mkono wa chuma, wanajiuliza mkono wa chuma hadi lini?

5. CCM wanaona uungwaji mkono hasa na vijana unazidi kuyoyoma, chuki dhidi ya chama inatamalaki na hilo litakula mtaji wao. Hofu , wakinamama wanakimbia kila uchao

6. CCM wanajua kitakachofuata kama si kesho ni kutwa au mwaka au miaka ni kisasi.
Vijana walioko madarakani wanajua na kwamba mbele ya safari watalipa gharama za kisasi.

Ungekuwa wewe , hiyo furaha unaipata wapi?

JokaKuu
 
Kuhusu Mbowe Toka Kwenye nafsi yangu kama mwana CCM ,,Hapana tunamtesa bure.hii ni Dhambi.
Mimi naona serikali inampapasa tuu,huyo alimdharau Rais waziwazi kwenye harakati zake za Katiba mpya na uhuru wa kujieleza.

Ngoja ashikishwe adabu kwanza,by the way anapanda kizimbani kwa hiyo ana haki ya kujitetea sio sawa na kama angewekwa korokoloni bila kupandishwa kizimbani.

Hapa Samia anastahili pongezi.
 
Yapo Mambo ukiyaangalia Kwa macho ya ROHONI unatambua Yana fumbo kubwa Sana. Mbowe ni mhalifu aliyekamatwa na serikali ya makini ya awamu ya sita,akafikishwa mahakamani...
Jaji hakuna alichosoma kwenye kesi hii. Haingii akilini kutumia siku mbili kusoma kurasa 1500 za proceedings. Huyu amejiaibisha na kuaibisha mfumo wa utoaji haki. Suala siyo kuamua Mbowe ana kesi ya kujibu, issue hapa ushahidi upi amezingatia kufikia maamuzi.

Kesi ya uchaguzi ya Kenya, Supreme Court chini ya CJ Maraga alitoa ruling pamoja na muda na kuwa mfupi, maana kikatiba kesi ya kupinga matokeo inatakiwa itolewe maamuzi ndani ya wiki mbili,hata CJ aliweza angalau kutoa summary kidogo kabla ya kutamka hukumu,huyu anajiumauma eti naona kama Kuna kesi ya kujibu,yeye mwenyewe ana mashaka.

Hata hivyo kwa mtu mwenye kufikiri mbali isingekuwa rahisi Mbowe kuachiwa hiyo jana, ingeleta implications nyingi kisiasa, yaani binafsi sikuwa naamini huyu jaji ni independent na bold kufanya maamuzi makubwa ya namna hiyo.
 
Jaji bwana. Kasoma kurasa 1500 kwa siku mbili.

Analipualipua tu kashaona serikali inamsumbua kwa kesi ambayo haipo.
Hata sisi wapenzi wa vitabu huwezi kusoma kitabu cha kurasa hata 800 tu kwa siku mbili.. haiwezekani. Maana kwenye hizo siku 2 kuna kulala,kula,kwenda chooni nk. Hii ni rekodi ya dunia. Bado hapohapo mtu apate na muda wa kuandika hukumu! Jaji alishapewa maelekezo
 
Mimi naona serikali inampapasa tuu,huyo alimdharau Rais waziwazi kwenye harakati zake za Katiba mpya na uhuru wa kujieleza.

Ngoja ashikishwe adabu kwanza,by the way anapanda kizimbani kwa hiyo ana haki ya kujitetea sio sawa na kama angewekwa korokoloni bila kupandishwa kizimbani.

Hapa Samia anastahili pongezi.
Amemdharau vipi?
 
Ni wanachama wa chadema ndiyo huwa wana kawaida ya kushangilia mabaya yanapowakuta wanachama wa vyama vingine!
Hivi ukiambiwa usipite njia hii kwani huko mbele kuna mbwa wakali wewe ukapuuza na kuporomosha maneno ya kejeli dharau kuonyesha ulivyojawa na kiburi, ukaendelea na safari yako. Ghafla unapiga kelele kuomba msaada kwa wale wale uliowadharau. Nini kitatokea hapo???
 
Mimi naona serikali inampapasa tuu,huyo alimdharau Rais waziwazi kwenye harakati zake za Katiba mpya na uhuru wa kujieleza.

Ngoja ashikishwe adabu kwanza,by the way anapanda kizimbani kwa hiyo ana haki ya kujitetea sio sawa na kama angewekwa korokoloni bila kupandishwa kizimbani.

Hapa Samia anastahili pongezi.
Kwa hiyo siyo Gaidi Bali Hana Adabu siyo???sasa mnampandisha kizimbani kujitetea Kwa kesi uliyokiri mwenyewe kuwa ni ya mchongo?? Yaani hakuna ugaidi Bali kumuweka mbali na madai ya KATIBA MPYA.
 
CCM ni watu wa ajabu Sana Yani Nchi Ina masikini hadi huruma lakini Hilo hawalioni kazi kufanya mambo ya kijinga tu .Sasa hivi nchi ipo gizani kwa Sababu hatuna umeme,bidhaa zimepanda bei Hilo hawalioni kazi kupoteza hela zetu walipa Kodi kwa makesi ya kubambikia watu.Tukienda hivi hatutafika na huu ni upumbavu,lakini yote Yana mwisho .
 
Back
Top Bottom