Kwanini viongozi wa kitaifa, wanasiasa wa CCM ,Wabunge na viongozi waandamizi Serikalini hawazungumzi wala kukemea utekaji nchini?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Mwaka 2024 umekuwa mwaka ulioibua utekaji na mauaji yasiyochinguzika.

Umekuwa mwaka wa kuzipiga vita 4R kwa minajili ya kukwamisha juhudi za maridhiano zilizokuwepo swali.

Umekuwa mwaka ambao vitendo vya kikatili vimeongezeka na kelele zimekuwa zikipigwa na wanasiasa na hata wananchi kama ilivyotokea Busega.

Lakini katika hali isiyo ya kawaida viongozi wa kitaifa awajawahi kunukuliwa wakikemea moja kwa moja na kutoa maelekezo ya kusitishwa kwa hiki kinachoendelea. Viongozi wa CCM pamoja na Bunge wapo kimya hakuna kauli thabiti ya kulaani inayotolewa.

Je, wanadhani watekaji wataishia kuteka maskini na wasio na utetezi au ipo siku watahamia kwa familia za vigogo wa Kiasia na utumishi wa umma. Tusipowadhibiti sasa tutaweza kuwadhibiti watakapofanya tukio kwa viongozi wa chama na serikali?

Ukimya wa mamlaka unaashiria nini? Au si wakati sahihi wakusema?
 
upotoshaji wa mchana kweupeee namna hii ni aibu na fedheha ya wazi wazi yenye ishara ya chuki binafsi na lengo la kuhamasisha chuki dhidi ya CCM na wananchi kwa ujumla na kutafuta huruma ambayo haina maana yoyote 🐒
 
Huwezi kusukuma gari ukiwa ndani yake!
 
Yanayotokea sidhani kama ni kwa bahati mbaya, wangeshupalia hilo jambo kama wanaobaka sidhani kama utekaji ungeendelea
 
Wanaopanga utekaji watakemea vipi utekaji?

4Rs ni.

1. Rabsha
2. Rafu
3. Risasi
4. Rambirambi
 
Kwani yule jamaa wa Bukoba aliyekuwa anajitapa kwa kazi hiyo alifanywaje ??!
Aliwaambia jamaa eti wawe wanafumba macho 😳🙄😱
 
Kujitekenya na kucheka ni ngumu
 
Wanasema huu utekaji/watu kupotea ni drama.
 
Hahaha.....mdomo koma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…