Kwanini viongozi wa Simba hawataki wazee waende kambini?

Kwanini viongozi wa Simba hawataki wazee waende kambini?

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Mzee Dalali ameomba wazee waruhusiwe kwenda pale kambini kuondoa upumbavu wote uliowekwa ambao unasababisha wachezaji waonekane hawana uwezo, wazito na hawajui mpira, wachezaji kama Chama, Bocco Baleke, Saido hawa hivi sio viwango vyao, hawa wamefanyiwa dawa wasitambe kabisa dimbani

Wazee wanaomba waruhusiwe wafike pale wakakague mazingira, wamesema yeyote aliyepiga misumari wachezaji wako tayari kumuangamiza, wenzenu kule Avic wanafanya kufuru, nyie leteni uzungu, mechi na Wydad ndio itakuwa alpha na omega kwetu, sare mbaya, kufungwa mbaya.

Mzee Dalali kama hawataki wenye simba yenu kwenda pale nyie nendeni t sisi tunataka ushind j4
 
Mzee Mangungu sijui Mangungo anatosha....[emoji41]

Dalali naye ni walewale wa maono ya Ndugu Rage...

Tabulele Fc .....tumieni akili, timu lenu bovu lina Wachezaji wazee na waliochoka..

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
 
Chief mangungo ndio kirusi chenyewe kwenye timu akinyofolewa yule timu itapumua
 
Mzee Dalali ameomba wazee waruhusiwe kwenda pale kambini kuondoa upumbavu wote uliowekwa ambao unasababisha wachezaji waonekane hawana uwezo, wazito na hawajui mpira, wachezaji kama Chama, Bocco Baleke, Saido hawa hivi sio viwango vyao, hawa wamefanyiwa dawa wasitambe kabisa dimbani

Wazee wanaomba waruhusiwe wafike pale wakakague mazingira, wamesema yeyote aliyepiga misumari wachezaji wako tayari kumuangamiza, wenzenu kule Avic wanafanya kufuru, nyie leteni uzungu, mechi na Wydad ndio itakuwa alpha na omega kwetu, sare mbaya, kufungwa mbaya.

Mzee Dalali kama hawataki wenye simba yenu kwenda pale nyie nendeni t sisi tunataka ushind j4
Hawa wazee na mawazo yao ya ushirikina "watukome"!! Wasipewe kabisa nafasi!! Karne ya 21 na mambo ya ushirikina wapi na wapi? Hawa wazee wasiruhusiwe kabisa kufika kambini!! Wakitaka kuwaona wachezaji, waende uwanjani wakawashangilie!! Haiwezekani sisi tunamwomba Mungu ili timu ishinde halafu atokee mshirikina adai timu imeshinda kwa ushirikina wake!! Wazee hawa washindwe na ushirikina wao kwa Jina la Yesu Kristo!! Utukufu wote tunampa Bwana Yesu!!
 
Mpira ni sayansi sio uchawi
Upewe maua yako!! 🥲🥲🥲🥲🥲. Hawa wazee wapigwe marufuku kabisa kwenye kambi!! Naami kwa ushirikina wao ndo walisababisha tupigwe mkono na uto!!
 
Chief mangungo ndio kirusi chenyewe kwenye timu akinyofolewa yule timu itapumua
Mzee Mangungu ANAHUJUMIWA na anafahamu hayo. Hao wazee hawakwenda kwenye mechi ngao ya hisani na Simba wakashinda. Pia hawakwenda mechi na El Ahl Simba hakuaibisha. Baadaye wakaenda na MO ktk kile kilichoitwa kamati ya kumshauri MO namna ya kuiongoza Simba matokeo yake kila mmoja anafahamu. Baada ya hapo MO na kamati yake wakawa mstari wa mbele kutaka Mangungu aachie ngazi. Je huyu mzee Mangungu ni juha kiasi gani asijifunze jambo kwenye mchezo huo?
 
Back
Top Bottom