Kwanini viongozi wa Tanzania wanapenda ziara za nje kuliko hata raia wake?

Kwanini viongozi wa Tanzania wanapenda ziara za nje kuliko hata raia wake?

Zygot

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2016
Posts
2,265
Reaction score
2,919
Hii ndiyo tabia ya viongozi wetu kupenda kusafiri, kuiona dunia. Yaani hata wanatafutiwa Ndege kwa ajili ya safari tu! Hiyo ni kazi ya maendeleo ya Taifa?

Wakati MV Bukoba inazama mwaka 1996, waziri mkuu wa Taznzania Ndg. Sumaye alikuwa ziarani Kusini mwa Afrika. Ikatangazwa ni janga la kitaifa, lakini waziri mkuu hakurudi nyumbani. Aliendelea na ziara na kula bata. Tangu hapo hakupendwa tena na wa-TZ inagawa rais Mkapa kwa kiburi chake alimrudisha ili kuwakomoa wa-TZ. Eti baadaye alipohama CCM, huyohuyo Mkapa akasema ni mpumbavu!

Mara hii tena Kariakoo kuna janga la kuanguka kwa gorofa. Katikati ya uokoaji, raisi amepunga mkono na kuelekea Brazil bila kujali kuwepo kwa janga hilo. Anatuma salamu za rambirambi akiwa ugenini, safarini, huku tunasema ni mama.

Tufanyeje ili tupate viongozi wanaojitambua?
 
Hii nimeona kule mtandaoni watu wakiijadili sana! Kuna shida kwa viongozi wetu. Imelinganishwa na tukiio la juzi ambalo waziri mkuu wa Uholanzi aliahirisha ziara ya kwenda mkutano wa kimataifa kwa sababu ya vurugu zilizofanywa na mashabiki wa mpira tu.

Sisi hawa wa kwetu wanawaza kwenda kuona beach za brazil wakati hata kwenye mkutano hawaonekani, na michango yao haifahamiki.
 
Back
Top Bottom