Kwanini Viongozi wetu wa Kisiasa hawaombi msamaha wanapokosea?

Kwanini Viongozi wetu wa Kisiasa hawaombi msamaha wanapokosea?

wanakiburi cha madaraka na kwamba wanajua wananchi tuko weak hatuwezi kufanya lolote kuhusu makosa yao.
 
kuna wakati nimewahi kufikiri kwamba viongozi wetu wamewahi kutumia 'bange' au mihadarati fulani ujanani mwao!

Mtu anaposema:
-HIVYO NI VIJISENTI TU

-NCHI IKIKAA GIZANI TUSILAUMIANE

-BORA WANANCHI WALE HATA NYASI ,LAKINI NDEGE YA RAIS LAZIMA INUNULIWE

lol!

Na hasa hawa wa sisi maf......😕
 
Viongozi wetu hawaombi msamaha kwa vile si wanyenyekevu. Wamejaa majivuno na majigambo. Pili, hawaombi msamaha kwa vile hawatuheshimu sisi waongozwa. Mtu usiyemheshimu si rahisi kumwomba msamaha. Unamwomba msamaha yule unayemheshimu, unayetambua utu wake. Kumbe wao wanatuona sisi watu wa kuja tu, tena tusio na uelewa mkubwa wa mambo
 
Kama Viongozi hawawajibiki na wanatumia fedha kupata kura ni nini sasa kifanyike?tukatae fedha zao au tule fedha zao na tusiwape kura 2010.
 
Si kwamba ni sisi wananchi ndio tunawalea kwa kutowawajibisha?
 
Back
Top Bottom