Viongozi wetu hawaombi msamaha kwa vile si wanyenyekevu. Wamejaa majivuno na majigambo. Pili, hawaombi msamaha kwa vile hawatuheshimu sisi waongozwa. Mtu usiyemheshimu si rahisi kumwomba msamaha. Unamwomba msamaha yule unayemheshimu, unayetambua utu wake. Kumbe wao wanatuona sisi watu wa kuja tu, tena tusio na uelewa mkubwa wa mambo