Kwanini vitabu vya dini vilikataza baadhi ya wanyama kuliwa?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Kwa Wakristo katika agano la kale ambalo bado linazingatiwa kwa kiasi kikubwa na Wasabato kuna wanyama walikataza kuliwa maarufu zaidi akiwa nguruwe/kitimoto wengine ni kama Sungura na ngamia. Samaki Kambale nao walikatazwa.

Kwa Waislamu wao najua nguruwe/kitimoto ndiye mnyama maarufu zaidi mwenye katazo la kuliwa, sijui kama kuna wengine.

Ni kwa nini hasa hawa wanyama walikatazwa kuliwa katika hivi vitabu vya dini?
 
Waafrica tulikula sana ngedere hao wakatuletea vijigonjwa gonna

Ingawaje naamini syphilis ililetwa na wqzungu
 
Ni kwa sababu.
Vitabu vya mungu vipo mbele ya MUDA.
Mungu alijua madhara ya kula hizo nyama ndo maana akakataza
Madhara ya kula nyama ya ngamia ni yapi??
 
Mzee
Unaweza kupata anthrax/kimeta kutoka kwa ng'ombe, mbuzi na kondoo ambao hawajakatazwa kuliwa.
KATAZO HALIKO KWENYE KULA KULA TU KASOME VIZURI
hizo ni kanuni za afya walipewa hao waebrania ambazo ni very practical mpaka leo
 
Kwa Wakristo katika agano la kale ambalo bado linazingatiwa kwa kiasi kikubwa na Wasabato kuna wanyama walikataza kuliwa maarufu zaidi akiwa nguruwe/kitimoto wengine ni kama Sungura na ngamia. Samaki Kambale nao walikatazwa.

Kwa Waislamu wao najua nguruwe/kitimoto ndiye mnyama maarufu zaidi mwenye katazo la kuliwa, sijui kama kuna wengine.

Ni kwa nini hasa hawa wanyama walikatazwa kuliwa katika hivi vitabu vya dini?
Baada ya gharika majani yalipotea,!Mungu akaruhusu baadhi ya mifugo kukiwa ,mambo ya walawi 11.Hamna Cha kuhoji.
 
Kwa Wakristo katika agano la kale ambalo bado linazingatiwa kwa kiasi kikubwa na Wasabato kuna wanyama walikataza kuliwa maarufu zaidi akiwa nguruwe/kitimoto wengine ni kama Sungura na ngamia. Samaki Kambale nao walikatazwa.
Kwahiyo biblia huwa inafanyiwa amendment mara kwa mara? Tutegemee kilicho katazwa sahivi huko mbele kinaweza kuruhusiwa? Kama alivyokatazwa nguruwe awali ila sasa analiwa?
 
Neno lenyewe biblia lilianza kutumika karne ya tatu AD, huko nyuma ilikuwa ni magombo, nyaraka au maandiko. Hata hivyo huu sio mjadala wa huu uzi, jikite kwenye mada.
 
Ndio.kwani alikula?
Aliingia nae sababu alitaka kuokoa vizazi vya wanyama.
Mi nimeuliza tu aliingia na nguruwe kwenye safina? Jibu ni simple ndiyo au hapana. Tunaeleweshana siyo kupanikishana

Swali lingine kama nguruwe ni najisi...kwenye Safina Nabii Nuhu alikuwa anaswali na nguruwe angali humo ndani?
 
Back
Top Bottom