Kwanini vitu vinapanda bei sana siku hizi?

Kwanini vitu vinapanda bei sana siku hizi?

Pole na majukumu wa Tanzania wenzangu kwa kulijenga taifa letu.

Jamani huku kwetu mkoa wa Songwe sasa ndoo ya mafuta ya kupikia elfu themanini nayo ni Toka nchi jirani ya kwetu ni elfu themanini na tatu na hayapatikani .sukari ya Tanzania Hamna kabisa napo ukibahatika ni tsh 3,500kg..
Mitano tena
 
Pole na majukumu wa Tanzania wenzangu kwa kulijenga taifa letu.

Jamani huku kwetu mkoa wa Songwe sasa ndoo ya mafuta ya kupikia elfu themanini nayo ni Toka nchi jirani ya kwetu ni elfu themanini na tatu na hayapatikani .sukari ya Tanzania Hamna kabisa napo ukibahatika ni tsh 3,500kg...
vitu vinapanda bei kwasababu uzalishaji wa hivyo vitu ni mdogo hivyo havipatikani kwa wingi. Sasa kwa kuwa havipatakani kwa wingi basi uhitaji unakua ni mkubwa mno.

Sasa kwanini havizalishwi kwa wingi yawezekana wazalishaji Hawana uwezo wa kuzalisha kukidhi Idadi ya wahitaji. Lakini pia
Gharama za uzalishaji na uendeshaji kuwa kubwa zinaweza kupelekea wazalishaji kuongeza bei ya kuuzia ili wapate faida inayoeleweka.

Kwasababu tunapo tafuta bei ya kuuzia tunahusisha gharama zote tulizo tumia kununulia mali ghafi, gharama za kuwalipa wafanyakazi na vibarua, gharama za kuendeshea mitambo ya kuzalisha, gharama za usafiri, kodi na faida tunayo itaka. Kwa hivyo ndugu yangu mchakato uko hivi.

Kwa hivyo hili swala linahitaji uchambuzi wa kiuchumi zaidi ili ipatikane sababu iliyosababisha.
 
Pole na majukumu wa Tanzania wenzangu kwa kulijenga taifa letu.

Jamani huku kwetu mkoa wa Songwe sasa ndoo ya mafuta ya kupikia elfu themanini nayo ni Toka nchi jirani ya kwetu ni elfu themanini na tatu na hayapatikani .sukari ya Tanzania Hamna kabisa napo ukibahatika ni tsh 3,500kg....
Mitano Tena
 
Mbona mnashindwa kuiokia jamii yenu dhidi ya sera mbovu zinazosimamia uchumi? Ushuru umekuwa kero utadhani kufanya biashara ni dhambi. Thamaani ya shilingi imefubaa. Waheshimiwa mliopewa thamana nijibuni. Si wengine mko bungeni ijapo hamna vyama vilivyo wateua kushiriki bunge? Mlipata tu ki-adventure? Hebu nijibuni.
 
Babu yenu mkulima hana furaha. Bei ya mbolea iko juu,bei ya mazao yake hapangi yeye, wanapanga walewale waliomuuzia mbolea kwa bei yakinyonyaji. Wasomi wanguhebu jitadhiminini. Kweli mnasababu ya kuendelea kuwepo mjengoni . Upo wapi ule ufaulu wenu wa A? Mjue Mungu anawaona.
 
Huko mjengoni kwenyewe kuna wasomi kweli, au kuna mabingwa tu walio kariri masomo darasani na kufaulu, na pia wale mabingwa wa kununua shahada za uzamili na uzamivu kwa kutumia hela zitokanazo na posho za vikao?
 
Back
Top Bottom