PostGE2025 Kwanini Vyama vya Upinzani vya Namibia Vinapinga Uteuzi wa Jaji Petrus Damaseb katika Tume ya Tanzania?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,914
Reaction score
168,320
1000030258.jpg

Ameandika Dr. Godbless Charles

Uteuzi wa Naibu Jaji Mkuu wa Namibia, Jaji Petrus Damaseb, kuwa mjumbe wa Tume ya Rais wa Tanzania ya kuchunguza matukio ya vurugu yaliyotokea kabla na baada ya uchaguzi umeibua mjadala si Tanzania pekee, bali pia nchini Namibia. Kinachovutia zaidi ni kwamba ukosoaji mkali umetoka kwa vyama vya upinzani vya Namibia, ambavyo vinaona uteuzi huo unaweza kuathiri hadhi ya mahakama ya nchi yao na hata uaminifu wa tume yenyewe.

Hoja ya kwanza inayotolewa na vyama hivyo ni kwamba jaji anayehudumu katika nafasi ya juu kabisa ya mahakama hapaswi kuhusishwa na uchunguzi wa kisiasa katika nchi nyingine, hasa pale ambapo mazingira ya kisiasa yanabishaniwa. Kwa mtazamo wao, hatua hiyo inaweza kuifanya mahakama ya Namibia ionekane imeingizwa katika mgogoro wa kisiasa wa taifa jingine badala ya kubaki taasisi huru ya utoaji haki.

Chama cha Affirmative Repositioning (AR) kimeeleza kuwa ushiriki wa Jaji Damaseb unaweza kudhoofisha taswira ya uhuru wa mahakama ya Namibia. Kimehoji kwa nini Naibu Jaji Mkuu wa nchi apelekwe katika tume ambayo tayari imegubikwa na mjadala wa kisiasa na madai ya ukiukaji wa haki za binadamu. Kwa mujibu wa chama hicho, hata kama jaji mwenyewe ni mwadilifu, mazingira ya uteuzi wake yanaweza kuathiri imani ya wananchi kwa taasisi ya mahakama.

Hoja ya pili ni kuhusu uwazi wa mchakato. Chama cha Independent Patriots for Change (IPC) kimehoji kwamba wakati Jaji Damaseb alipokubali uteuzi huo, masharti ya rejea (Terms of Reference) ya tume hayakuwa yamewekwa wazi hadharani. Kwa mtazamo wa IPC, ni vigumu kwa jaji wa ngazi hiyo kukubali jukumu ambalo mamlaka yake, upeo wake na mipaka yake haijafafanuliwa kwa umma.

IPC imeenda mbali zaidi kwa kusema kwamba Namibia ilipaswa kwanza kuzungumzia hadharani madai ya ukiukaji wa haki za binadamu nchini Tanzania kabla ya kushiriki katika tume ya uchunguzi. Kwao, kutuma jaji wa hadhi ya juu bila kwanza kuonyesha msimamo kuhusu tuhuma hizo kunaweza kutafsiriwa kama kuipa tume uhalali wa kimataifa kabla haijathibitisha uhuru wake.

Hata hivyo, IPC ilisisitiza wazi kuwa haikuwa ikihoji uadilifu wa Jaji Damaseb binafsi; ilimwelezea kuwa mmoja wa majaji bora wa Namibia, lakini ikaonya kwamba sifa yake inaweza kutumiwa kuongeza uaminifu wa tume ambayo uhuru wake bado unaulizwa.

Kwa hiyo, mjadala uliopo Namibia haujajengwa juu ya madai kwamba Jaji Damaseb si mwadilifu. Badala yake, umejengwa juu ya kanuni muhimu ya utawala wa sheria kwamba taasisi za mahakama zinapaswa kulindwa dhidi ya mazingira yanayoweza kuzifanya zionekane zimejihusisha na migogoro ya kisiasa.

Kwa Tanzania, hoja hii ina umuhimu mkubwa. Tume inayochunguza matukio yaliyotokea baada ya uchaguzi inatarajiwa kurejesha imani ya wananchi. Hilo haliwezi kutegemea tu uwezo wa wajumbe wake, bali pia namna wanavyoonekana machoni mwa umma na uwazi katika namna walivyopatikana.
Endapo hata katika nchi anayotoka mmoja wa wajumbe kuna vyama vya kisiasa vinavyohoji uhalali wa ushiriki wake kwa misingi ya taswira ya uhuru wa mahakama, ni jambo linalostahili kujadiliwa kwa uzito.

Mwisho, swali ambalo Watanzania wanaweza kujiuliza si kama Jaji Petrus Damaseb ana uwezo wa kitaaluma. Swali ni kama uteuzi wake, katika mazingira haya ya kisiasa, unajenga au unapunguza imani ya wananchi kwa tume iliyokusudiwa kutafuta ukweli na kuleta maridhiano. Katika tume za uchunguzi, uhalali wa matokeo huanza na uaminifu wa mchakato na watu wanaouongoza.
 
View attachment 3645733

tume ya uchaguzi?

BBC wanaota au ni katika muendelezo wa harakati zao za kuzuia confusion za kila mara katika jamii?

kwahiyo wamewahoji watu wa Namibia kuhusu jaji wao kateuliwa kwenye tume ya uchaguzi Tanzania na sio tume ya uchunguzi, right 🐒
 
Saa100 ameshaichafu mahakama Tanzania, anataka kuichafua Namibia
Namibia wameshtuka!
 
Back
Top Bottom