Kwanini vyombo vya habari huwa hivioneshi magoli kwenye ligi yetu wakati wa kutangaza habari

Kwanini vyombo vya habari huwa hivioneshi magoli kwenye ligi yetu wakati wa kutangaza habari

Mapensho star

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2016
Posts
3,052
Reaction score
4,104
Huwa nashangazwa na jambo hili kwenye ligi yetu Tanzania mimi sio mfuatiliaji wa mpira mara nyingi nikiangalia taarifa za habari wasaa wa michezo huwa napenda kuangalia magoli yamefungwaje Lakini cha ajabu huwa nakutana na simulizi tu ya mchezo mzima ulivyotokea magoli siyaoni.

Tofauti na ligi za ulaya magoli yote yanayofugwa yanaoneshwa kwenye taarifa ya habari kwenye bbc news au cnn Sasa naombeni mnijuze wadau sijui kitu gani kinawakwamisha waandishi wetu sisi tunaopenda kuangalia magoli kwenye taarifa ya habari tunakosa uhondo
 
Usikose mashindano ya bonanza na kriketi wiki hii mkuu.
ITV inabidi wafanyie kazi kitengo chao cha michezo.... Star TV na ubovu wao lakini Michezo na habari za kimataifa wanawakimbiza
 
Hii changamoto niliiona mapema sana.
Lkn hakuna poa kusemea. Wao ndio wana taaluma ya habari labda wameambiwa hivyo🤷🤷🤷🤷
 
Huwa nashangazwa na jambo hili kwenye ligi yetu Tanzania mimi sio mfuatiliaji wa mpira mara nyingi nikiangalia taarifa za habari wasaa wa michezo huwa napenda kuangalia magoli yamefungwaje....
MARA NYINGI:TV zilizolipa malipo ya kuonyesha mpira,zinakuwa na haki ya kuonyesha mpira"Live",wale ambao hawakulipia wanaweza kumlipa fedha yule aliyepata haki ya kurusha matangazo mubashara.

Kwa hiyo yawezekana TV zinakwepa kuonyesha magoli itakujakuwapa shida kwa vile itaonekana hawajawasiliana na "mwenye haki ya kuonyesha mpira mubashara"
 
Habari za michezo huwa ni vituko vingi sana. Kama ulivyosema unaweza kuta labda Mtibwa kashinda 4-0 lakini reporter atabwabwaja hapo mpaka habari inaisha huoni goli hata moja au linaoneshwa moja na kujirudia hilo hilo.

Media kubwa kama ITV kwenye habari za michezo ni chenga kabisa. Habari za kuokoteza na video pia za kuunga unga.
 
Hii kweli ipo katika mambo ya copyrights. Mfano kwenye habari za michezo za Sky News wanaonesha kabisa magoli ya ligi kuu England, lakini BBC wao wanaonesha matokeo tu na still pictures.

Ila huku kwetu ni tofauti kwa sababu wataoneshwa watu wanakimbia wanacheza mpira tena camera yenyewe inakua kama ya simu vile imezoom [emoji1][emoji1][emoji1].
 
Azam media ndio ana rights za mpira WETU, TV zote inabidi ziombe clip kwa azam, inawezekana Azam haitoi hizo clip aka TV hawaombi hizo clip
 
huyu ni mpenzi mtamazamaji wa ITV/TBC
Watakuwa Wanaogopa kuomba clip za azam sababu wao wanasema ni superbrand kumbe wanafeli

Back
Top Bottom