Kwanini vyombo vya magharibi ikiwemo Ufaransa vinalalamika kukamatwa kwa wanajeshi wa M23 Tanzania? Wananufaikaje na mgogoro wa Congo?

Safi sanaaaaaa
 
Jina lako linasadifu ulichokiandika.
 
Kuwaachia waasi kuja bongo na kujinafasi ni sawa umuone nyoka wa jirani yako kaingia room kwako halafu useme hamna shida!

Tanzania ina jukumu la kusaidia DRC kukomesha uasi na kuua wote wanaoshambulia mashariki ya Congo maana waasi wa M23 wakitamalaki DRC wakapata nguvu kubwa watasaidiwa na Rwanda na Uganda zisiyo na rasilimali wala bandari kuvamia bongo , tulimuona Idi Amin.

Huwa inasemwa ukila nyama ya mtu huwezi kuacha, M23 wakikamilisha mission ya DRC watawaza sehemu ingine na si ajabu wakiichagua bongo na kuivamia!! Siku zote ogopa sana mtu masikini aliekamata bunduki huwa hana cha kupoteza, ingependeza bongo kuongeza vikosi DRC maana ni kwa faida ya bongo pia kuua na kutokomeza waasi wa M23 maana wana hasira pia na bongo kwa kulinda amani DRc kwa miaka mingi

Waasi wa M23 ni hatari kwa usalama wa nchi zote za maziwa makuu. Hawa ni wa kutokomeza na kuogopa kama ukoma, mwenzako akinyolewa we tia maji!!


Tz ni nchi huru haipaswi kupangiwa cha kufanya katika kulinda usalama wake, kukamata waasi na kuwakabidhi DRC ni sahihi kabisa. Yaani nchi ifuge magaidi wa Congo hiyo hakuna!
 
Ivi wewe mwandishi umeandika Nini sasa .yaani unataka useme watanzania wote tunafurahia ukiukaji haki za binadamu.nikuuze huyo muasi amekatwa DRC au Tanzania.je sisi Tz tumetangaza vita na M23.kama sio .basi tumekiuka Sheria za kivita na haki za binadam.Afalu makosa ya M23.hayatupi garantii ya kujiingiza vita M23
 
Kusoma Kwa kukalili
,huyo jamaa ni mkombozi??
 
Haki gani za kibinadamu zimekiukwa!?
Kwani hao ni wakimbizi au waasi!?
Yani muasi atoroke aingie nchini halafu umuache!?
Hufai kuwa kiongozi wewe maana utateteresha amani ya nchi.
 
Sio hilo tu la kuwazuia M23 kukimbilia nchini mwetu. Tuzuie bandari zetu kutumika kuingiza silaha kwa majeshi ya Rwanda. Tuko Congo kupigana na nani kama sio Rwanda ambayo ni mwanzilishi wa fujo maziwa makuu na mvamizi congo. Pia tanzania inafaa kumkataa balozi mpya wa rwanda anayependekezwa na Kigali. Huyo ni jasusi na atatumia nafasi hiyo kuhujumu mipango yetu ya usalama. Hao watu wamejaa hila mbaya kupindukia tuwe makini sana kuhusu wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…