Kwanini Waafrika Tunadharauliana Wenyewe Kwa Wenyewe?

MwendaOmo

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2013
Posts
774
Reaction score
723
Yaani kama kuna jambo ambalo hunikera mimi ni kuona jinsi sisi waafrika tunadharauliana wenyewe kwa wenyewe. Kile kitu ambacho huwezi ukamfanyia mzungu, unamfanyia mwafrika bila hata kujali. Kwanini tunajichukia kiwango hichi? Hatujui kuwa watu wa rangi zingine zote wanatudharau?

Kuhusu ile kesi ya wanahabari kuenda TZ, mmoja alikuwa mweusi mkenya na mwengine alikuwa Mzungu wa SA. Nilipojua kuwa mzungu yupo kati yao, nilijua tu waachiliwa haraka. Sasa TISS (Yaani TISS inajihusisha na mambo kama haya?) Baada ya kuwakamata hawa watu, walikuwa wakali sana kwa mkenya, na kumtusi na hata kumpiga. Ilhali mzungu hakuguswa. Soma hapa

Hili ni jambo ambalo linasikitisha sana. Kwanini tuko hivi? Ukiwa SA, TZ, Congo, Nigeria au Hata Kenya, waafrika kwa waafrika tunafanyiana maovu ambayo hatuwezi tukamfanyia mzungu. Kweli tuko taabani.
 
Sikuwa nimeona ule uzi mwingine. mr mkiki Sidhani kama ni utawala. Yaani utawala wa sasa umewafanya hawa watu roho zao zikaonekana. Hadi mzungu anaiita Afrophobia. Siku moja watamfanyia hivyo back American ndiposa watazitambua nchi ambazo zinawapenda wananchi wao.
 
Don't use one situation and conclude stuffs. Returning to ur question ,Ni tatizo la kimfumo wengi hujikuta wakifanya hivyo bila kujua . But i have to say this kuna baadhi ya nchi ni zaidi( They hate 4 no reason) , Wakenya mnisamehe kwa hilo but i have personally witnessed this kwa nchi yenu hili lipo sana. kwa bongo wengi chuki zinatokana na sababu ambazo ni za msingi.
 
Ujinga kutoka kwa watu kama Wadangagiza. They were brainwashed by Arabs.
Mnakumbuka wakenya mlivyomfanyia yule blogger wa Ghana anayeishi China anayeitwa MAYA?, aliposema anatoka Ghana, POLISI wa Kenya ndio walipozidisha mateso, hadi aliposema ana residence permit ya China ndipo walipolegea na kumwachia Uhuru.
 
Sababu gani za kimsingi zitakufanya umdharau na kumtendea Mwafrika mwenzio maovu huku ukimshobokea mzungu aliyekutia pingu na kukufanya kijakazi wake? Stop making excuses for mediocrity in the name of patriotism.
 
Are we the police? Are the police us?
Hahahahahaha, nyanyangu wakati mwengine huwa unanifurahisha sana, kwani hao waliowasumbua hao wana habari ambao tunawalalamikia ni raia wa kawaida?. Are we Tanzania Intelligent Security Service?
 
Sababu gani za kimsingi zitakufanya umdharau na kumtendea Mwafrika mwenzio maovu huku ukimshobokea mzungu aliyekutia pingu na kukufanya kijakazi wake? Stop making excuses for mediocrity in the name of patriotism.
Waulize wale POLISI wa Kenya waliomnyanya yule MAYA toka Ghana, hata baada ya kujitambulisha kwamba yeye ni Mghana lakini waliendelea kumsumbua hadi aliposema resident of China ndio walipomuachia, why?
 
Sababu ni kwamba > 80% ya Waafrika (weusi) hatulelewi na Upendo, Waafrika wengi wamelelewa na Ukatili, hivyo kama mtoto akilelewa na Mzazi mkatili ambaye humpiga na kumuadhibu kama apigavyo ngoma, basi mtoto hukuwa akiamini kwamba yeye hastahili mambo mema na mazuri na kwamba ni sawa kwake kupata shida, ndo maana Mwafrika hupendelea Muzungu, Muhindi, Mwarabu au hata chotara kuliko yeye mwenyewe.

Hivyo ni malezi tu hakuna miujiza na kama ukitaka kubadilisha hili mpende mtoto wako, mueonyeshe upendo wa dhati usimpige kama ngoma na wala usiruhusu mtu yoyte yule ampige au kumnyanyasa awe Mwalimu au sijui jirani au rafiki yako na msikilize akiwa na shida umsadie, utapunguza kizazi kisichojipenda na kijithamini!

Tanzania wanapiga watoto hadi wanauwa, na kuna watu wanajisifia kwamba yeye anapiga mtoto hadi anashika adabu, sasa mtoto anayelelewa hivi anawezaje kujiependa na kujithamini?

 
Waulize wale POLISI wa Kenya waliomnyanya yule MAYA toka Ghana, hata baada ya kujitambulisha kwamba yeye ni Mghana lakini waliendelea kumsumbua hadi aliposema resident of China ndio walipomuachia, why?
Hivi huko Tanzania mara ngapi Wafrika wamenyanyaswa bila sababu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…