Yaani kama kuna jambo ambalo hunikera mimi ni kuona jinsi sisi waafrika tunadharauliana wenyewe kwa wenyewe. Kile kitu ambacho huwezi ukamfanyia mzungu, unamfanyia mwafrika bila hata kujali. Kwanini tunajichukia kiwango hichi? Hatujui kuwa watu wa rangi zingine zote wanatudharau?
Kuhusu ile kesi ya wanahabari kuenda TZ, mmoja alikuwa mweusi mkenya na mwengine alikuwa Mzungu wa SA. Nilipojua kuwa mzungu yupo kati yao, nilijua tu waachiliwa haraka. Sasa TISS (Yaani TISS inajihusisha na mambo kama haya?) Baada ya kuwakamata hawa watu, walikuwa wakali sana kwa mkenya, na kumtusi na hata kumpiga. Ilhali mzungu hakuguswa. Soma hapa
Hili ni jambo ambalo linasikitisha sana. Kwanini tuko hivi? Ukiwa SA, TZ, Congo, Nigeria au Hata Kenya, waafrika kwa waafrika tunafanyiana maovu ambayo hatuwezi tukamfanyia mzungu. Kweli tuko taabani.