Kwanini Waafrika wengi wanapenda kulalamika?

Kwanini Waafrika wengi wanapenda kulalamika?

Mbahili

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
281
Reaction score
525
Mawasalimia kwa jina la jamhuri.

Leo nimeona nilete uzi mdogo hapa kwenu kwa swali nililoliwaza sana. Kwanini Waafrika wengi tunapenda lalamika? Hapo awali nilidhani tatizo ni umaskini, ila pia kwanini matajiri pia wanalalamika?

Nimepita baadhi ya nyuzi kibao huku, nimeona wengi wana express hoja inform of lawama, ooh hivi ooh vile, why? Kila mtu analalamika, kuanzia mtu wa chini mpaka viongozi why?

Nilijaribu kumuuliza rafiki yangu mmoja kuhusu huko kwao (mambele), kasema kuna malalamiko ila sio kama huku. Nimekuja gundua kuwa, it's our nature to complain, tumeumbwa tulalamike.

Unamkuta mtu anaamka saa 4 asubuhi analalamika maisha magumu, unakuta kiongozi hayuko responsible analalama wafanyakazi hawajitumi au sales ikishuka analaumu team.

Suluhisho la lawama. Chukua responsibility, kama wewe ndio kiongozi sector fulani, chukua responsibility either achia ngazi ila usilaumu.

Mtu wa chini, ukiona unataka uanze lawama, usifikirie hivyo either pambana ufike juu au pia acha kazi.
 
Back
Top Bottom