Kwanini Waalimu Tu,sio Wengine

Kwanini Waalimu Tu,sio Wengine

Adharusi

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2012
Posts
14,422
Reaction score
7,350
Mimi nashangaa lawama kibao kwa
"WALIMU"
Mbona mikoa isiyo na Chakula Maafisa KILIMO hawalaumiwi?Mbona RUSHWA imekithiri TAKUKURU hawalaumiwi? Wagonjwa kibao hufariki daily lakini MADAKTARI hawalaumiwi?
Kodi hazikusanywi ipasavyo mpaka nchi kuwa maskini lakini TRA hawalaumiwi? Je hii ni haki kweli?Walimu tumechoka lawama! Mtumie mwl yeyote unayemjua.
CC Madame B,Mamndenyi,Evelyn salt
 
Kwenye hiyo list, Ungewa-exclude madaktari..

Uhai ama kifo ni kudra za Mwenyezi Mungu....
 
Kama utawaondoa madaktari kwa kua kifo ni mpango wa mungu, basi usiwatuhumu walimu kwakua mungu ndio mpangaji wa kila kitu. Hata kufeli mitihani kwa mwanafunzi ni mpango wa mungu.
 
kwani na wewe umelazimishwa kuwa mwalimu , si uache ufanye hizo kazi nyingine unazoona hazina lawama ...
 
Kwenye hiyo list, Ungewa-exclude madaktari..

Uhai ama kifo ni kudra za Mwenyezi Mungu....

Sure mkuu, hata waje madaktari na Phd zao Mungu akishamuhitaji kiumbe wake hakuna wa kupinga.....
 
Kama utawaondoa madaktari kwa kua kifo ni mpango wa mungu, basi usiwatuhumu walimu kwakua mungu ndio mpangaji wa kila kitu. Hata kufeli mitihani kwa mwanafunzi ni mpango wa mungu.

Kuwahukumu na kuwatuhumu walimu siyo busara, lakini ni kheri kufanya hivyo kuliko kupiga kimya.

lakini lazima uhoji ktk massive failures, kwanini vijana wafeli wengi miaka hii ya karibuni ukilinganisha miaka ya nyuma...

Pia walimu wanaandamwa zaidi kwasababu wao ndio, ground roots wa kila fani, ukiona agriculturalist hayupo efficient katika kazi yake, basi yawezekana tatizo lilianzia kwa mwl.
 
kwani na wewe umelazimishwa kuwa mwalimu , si uache ufanye hizo kazi nyingine unazoona hazina lawama ...

Well said! Siamini kama kuna mtu amefungwa pingu za maisha kufanya kazi asiyoipenda. Mtu kama huridhiki na Maslahi ya Ajira uliyonayo, piga Ajira chini, nenda kwenye Ajira unayoipenda, kama unatimiza Vigezo!

Tunaishi kwenye Nchi yenye misingi ya Katiba inayoruhusu Mtu kufanya kazi anayoipenda ili mradi havunji Sheria.

Kubali usikubali, kuna Waalimu wanaoupenda Ualimu, wameridhika na Ualimu na wamefanikiwa katika maisha kwa Ualimu. Hivyo malalamiko yasiyoisha ya Watu walioshindwa maisha kwa kusingizia Ualimu ni kuwavurugia Waalimu hao.

Mwalimu ana fursa kibao za kufanikiwa akiamua. Moja ya fursa hizo ni muda. Wakati Mwalimu kwa kawaida anafanya kazi kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 10 jioni (kwa ujumla), j'tatu hadi Ijumaa, Mfanyakazi wa Benki, mfano, ni kawaida kupiga hadi usiku, J'tatu hadi J'pili. Hatujaongelea urahisi wa ruhusu za Kazi, Mikopo ya Riba nafuu ya NMB, n.k. Kwa ufupi, fursa ziko kibao!
 
Back
Top Bottom